Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Ituri: Watu 22 wamefariki katika mapigano kati ya FARDC na CODECO huko Mongwalu

Watu 22 wakiwemo raia kumi na watatu na wapiganaji wanane wa waasi waliuawa wakati wa mapigano ya siku mbili kati ya Jeshi la DRC (FARDC) na kundi la waasi la CODECO huko Mongwalu katika mkoa wa Ituri.

Wanajeshi wa DRC wakishika doria katika moja ya maeneo ya Djugu.
Wanajeshi wa DRC wakishika doria katika moja ya maeneo ya Djugu. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Jeshi lilipambana na washambuliaji hawa kuanzia Jumanne Agosti 30 hadi Jumatano Agosti 31 katika mji huu wa madini ulio kilomita 85 kaskazini mwa Bunia katika eneo la Djugu, mkoani Ituri.

Raia waliouawa ni wachimbaji madini ya dhahabu. Raia wengine wanne walijeruhiwa wakati wa mapigano haya, vyanzo vya ndani vinaripoti.

FARDC iliua wanamgambo wanane wa CODECO, akiwemo kamanda wa operesheni wa wanamgambo hawa, na wapiganaji wengine kumi na moja walijeruhiwa.

Kwa upande wa jeshi, mwanajeshi mmoja aliuawa, kulingana na vyanzo hivyo.

Uharibifu mkubwa wa vifaa vya jeshi pia unaripotiwa: karibu nyumba na maduka 60 zilichomwa moto na kituo cha polisi kiliharibiwa vibaya.

Wilaya nzima ya Mongwalu imekuwa chini ya udhibiti wa jeshi tangu Jumatano jioni. Jeshi linaendelea na doria katika eneo hili la madini, Radio Okapi nchini  DRC imerooti ikinukuu vyanzo kadhaa.

Mapigano yalianza tena Jumatano asubuhi kati ya pande hizo mbili na yalidumu karibu masaa 5.

Baada ya kushindwa dhidi ya jeshi, waasi wa CODECO walijiondoa kwenye ngome zao huko Brazil, Digene na Mbau, vyanzo hivyo vimeongeza.

Hata hivyo jeshi hilo linaendelea na msako katika mkoa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.