Pata taarifa kuu

Mashirika mawili yashutumu ‘kampeni ya maangamizi ya kikabila’ Tigray Magharibi

"Kampeni ya maangamizi ya kikabila" huko Tigray Magharibi nchini Ethiopia, hivi ndivyo mashirika mawili ya kimataifa ya Hki za Binadamu, Amnesty International na Human Rights Watch, yanalaani katika ripoti ya pamoja iliyotolewa siku ya Jumatano.

Kambi ya watu waliokimbia makazi yao iliyowekwa katika shule ya upili ya Mayweli, huko Mekele, mji mkuu wa mkoa wa Tigray nchini Ethiopia, Mei 2021.
Kambi ya watu waliokimbia makazi yao iliyowekwa katika shule ya upili ya Mayweli, huko Mekele, mji mkuu wa mkoa wa Tigray nchini Ethiopia, Mei 2021. © RFI / Sébastien Németh
Matangazo ya kibiashara

Eneo la utawala linalozozaniwa, lililokuwa chini ya utawala wa utawala wa Tigray tangu miaka ya 1990, Western Tigray liko chini ya udhibiti wa Jeshi la Kitaifa la Ulinzi la Ethiopia (ENDF) na vikosi vya washirika na wanamgambo kutoka eneo la Amhara katika kipindi cha wiki mbili baada ya kuzuka kwa mzozo huko Tigray mnamo mwezi wa Novemba 2020.

"Waliendelea kusema, 'Tutawaua. Ondokeni, nendeni nje ya eneo hili," amesema mwanamke mmoja kutoa jimbo la Tigray. Ushahidi huu ni mmoja wa mamia shahidi zilizokusanywa na wachunguzi kutoka Amnesty International na Human Rights Watch. Jumla ya shahidi 400 zilikusanywa na mashirika hayo. Ikiwa ni pamoja na shahidi wa raia mmoja wa Tigray mwenye umri wa miaka 70, aliyekamatwa huko Humera mwaka jana, anasema Laetitia Bader, mkurugenzi wa Human Rights Watch katika Pembe ya Afrika.

"Alizuiliwa kwa wiki 2 huko Bet Hintset, mojawapo ya vituo vya kizuizini visivyo rasmi ambapo tumeandika dhuluma mbaya zaidi huko Humera, pamoja na kile anachoamini kuwa maelfu ya wafungwa wengine. Alipigwa - mzee wa miaka 70 - mara kadhaa. Akiwa kizuizini, wanaume wawili wazee aliowajua walipigwa hadi kufa. Baada ya wiki mbili, na akiwa katika hali mbaya, alipakiwa kwenye lori na kusafirishwa hadi mto Tekeze. Baadaye, katika sehemu nyingine ya Tigray, mtu huyu alinusurika shambulio la ndege isiyo na rubani. Uhalifu huu mbaya sana unapaswa kuibua vilio na mwitikio wa kimataifa. Lakini kampeni hii dhidi ya watu wa Tigray imefichwa kwa ulimwengu sio tu kwa sababu ya nia ya mamlaka ya shirikisho na kikanda kuzuia upatikanaji wa watetezi wa haki za binadamu na vyombo vya habari huru, lakini pia kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa kwa jumuiya zinazowazuia kukimbia."

Baada ya miezi kumi na tano ya kazi ya pamoja, katika ripoti yao inayojumuisha takriban kurasa 250 za shuhuda za ghasia zisizo za kawaida, Amnesty na Human Rights Watch wameelezea kile walichokiita kama "kampeni iliyoratibiwa ya mateso yanayolengwa kwa maangamizi ya kikabila" dhidi ya wakazi wa eneo la Tigray Magharibi. "Mipango ya kuangamiza wakazi wa eneo la Tigray imejadiliwa na kuzungumzwa hadharani hususan katika mikutano, kupitia vipeperushi. Mamlaka pia imenyima jamii za watu kutoka Tigray rasilimali muhimu kwa maisha yao kwa kuwanyima kupata ardhi zao. Pia walihimiza uporaji, kwa kutoa vibali vya usafirishaji wa bidhaa zilizoporwa,” kulingana na Fisseha Tekle, mtafiti wa Amnesty International.

Mashtaka ya "uhalifu wa kivita" na "uhalifu dhidi ya binadamu"

Ripoti ya mashirika haya mawili imeonyesha orodha ndefu ya unyanyasaji: visa vya watu kuuawa bila kufikishwa mahakamani, unyanyasaji wa kijinsia, kukamatwa kiholela kwa watu wengi, pamoja na visa kadhaa vya watu kulazimishwa kuyahama makazi yao, ikiwa ni pamoja tukio kama hilo lililotokea mwezi wa Novemba mwaka jana.

Wachunguzi hao wanaandika hasa mauaji ya takriban watu sitini kwenye mto Tekeze, kufukuzwa kwa watu wengi kitendo kulichosimamiwa na mamlaka mpya ya kiraia au hata vituo vya kizuizini vya siri ambapo watu wa Tigray wanateswa na kuuawa.

Unyanyasaji huu unajumuisha, kulingana na mashirika haya mawilii, "uhalifu wa kivita" na "uhalifu dhidi ya binadamu". "Malori yaliyowabeba wakazi wa Tigray mara nyingi yalisindikizwa na vikosi maalum au wanamgambo wa Amhara, wakati mwingine na vikosi vya serikali ya shirikisho. Uratibu katika ratiba na miondoko ya mabasi, pamoja na mfanano katika shuhuda zinaonyesha kuwa hizi ni shughuli zilizopangwa na serikali kuu, "amesema Laëtitia Bader.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.