Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Waasi wa Tigray wakubali kusitisha vita kuruhusu misaada ya kibinadamu

Waasi wa Tigray nchini Ethiopia wamekubali hatua ya serikali kusitisha vita ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wakimbizi na watu wengine walioathiriwa na mzozo huo wa miezi 17.

Waasi wa Tigray nchini Ethiopia
Waasi wa Tigray nchini Ethiopia AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao, waasi hao wamesema wana nia ya dhati ya kuheshimu na kutekeleza hatua ya serikali ya Ethiopia, na kuitaka kuharakisha ili misaada hiyo iwafikie maelfu ya watu ambao wanaendelea kuteseka na wanahitaji chakula, maji, dawa na mahitaji mengine muhimu.

Siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alitangaza, serikali yake ilikuwa inasitisha mapigano yote na kuruhusu misaada ya binadamu kuwafikia wakaazi wa Tigray ambao wamesalia kuwa wakimbizi, hatua ambayo ameeleza pia kuwa, anaamini itasaidia kusuluhisha mzozo huo.

Hatua hii ya serikali nchini Ethiopia, imepongezwa na Umoja wa Mataifa, Marekani, Umoja wa Ulaya na ule wa Afrika huku wito ukitolewa kwa pande zote kutumia nafasi hii kufanikisha mazungumzo ya kutatua mzozo huu.

Tangu kuzuka kwa mapigano katika jimbo la Tigray mwezi Novemba mwaka 2020, maelfu ya watu wameuawa na wengine kuyakimbia makwao, baada ya mzozo huo kusambaa kutoka Jimbo la Tigray na kufika katika majimbo ya Amhara na Afar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.