Pata taarifa kuu
RIADHA-DUNIA-ETHIOPIA

Ethiopia yaongoza dunia mashindano ya ndani ya riadha

Mashindano ya riadha ya dunia ya ndani, yamemalizika mjini Belgrade, nchini Serbia kwa Ethiopia kumaliza ya kwanza duniani kwa medali tisa.

 Yomif Kejelcha, bingwa wa zamani wa mbio za Mita 3,000 katika mashondano yaliyopita
Yomif Kejelcha, bingwa wa zamani wa mbio za Mita 3,000 katika mashondano yaliyopita AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Nne za dhahabu, tatu za fedha na mbili za shaba. Miongoni mwa wanariadha wa Ethiopia, walioshinda medali za dhahabu ni pamoja na Samuel Tefera katika mbio za Mita 1500, Selemon Barega mbio za Mita 3000 kwa upande wa wanaume.

Marekani ilimaliza ya pili, kwa medali 19.Tatu za dhahabu, saba za fedha na tisa za shaba.

Kenya, ilimaliza ya 22 baada ya kupata medali mbili, moja ya fedha na nyingine ya shaba.

Noah Kibet aliipatia nchi yake medali ya fedha katika mbio za Mita 800 huku Abel Kipsang akimaliza katika nafasi ya tatu, katika mashindano ya mbio za mita 1500 kwa upande wa wanaume.

Bonyeza hapa kuangalia namna nchi mbalimbali zilivyopata medali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.