Pata taarifa kuu

Sudan: Klabu ya Al Hilal kushiriki katika ligi kuu ya Tanzania

Nairobi – Mamlaka nchini Tanzania imekubali kuiruhusu klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan kushirika katika ligi kuu ya taifa hilo wakati huu ambapo mapigano yanaendelea huko Sudan.

Klabu hiyo haitakuwa na uwezo wa kushinda taji la ligi ya Tanzania na itashiriki tu mechi za ligi kama za kirafiki
Klabu hiyo haitakuwa na uwezo wa kushinda taji la ligi ya Tanzania na itashiriki tu mechi za ligi kama za kirafiki © Getty Images/iStock/Artisteer
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Al Hilal itashiriki katika ligi kuu ya Tanzania kuanzia mwezi Agosti kwa vigezo maalum.

Klabu hiyo haitakuwa na uwezo wa kushinda taji la ligi ya Tanzania na itashiriki tu mechi za ligi kama za kirafiki.

Msemaji wa shirikisho la soka nchini Tanzanian Clifford Mario Ndimbo, amewaambia wanahabari kuwa ushiriki wa Al Hilal utakuwa na manufa kwa ligi yao.

Aidha Clifford ameongeza kuwa waamuzi wa Sudan walioko nchini Tanzania watapewa nafasi ya kusimamia mechi kadhaa za ligi.

Al Hilal ilitoa ombi la kuruhusiwa kushiriki katika ligi ya Tanzania kutokana na michezo kupigwa marafuku nchini mwao kutokana na mapigano kati ya pande mbili za kijeshi.

Mamia ya watu wameuawa katika mapigano hayo yaliozuka mwezi Aprili mwaka jana, mamilioni ya wengine wakipoteza makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.