Pata taarifa kuu
WRC Safari Rally 2024

Kalle Rovanpera aibuka na ushindi mkubwa kwenye WRC Safari Rally

Naivasha – Bingwa wa msururu wa WRC mara mbili (2022 na 2023), Kalle Rovanperä ameibuka mshindi wa makala ya mwaka huu ya kuendesha magari ya WRC Safari Rally kwa kuhitimisha mkondo huo wa Afrika kwa ushindi wa dakika moja na sekunde 37.8 akiwa ameongoza tangu Ijumaa asubuhi.

Kalle Rovanpera na msaidizi wake Ferm Janne wa Toyota GR Yaris wakisherehekea ushindi wa Safari Rally 2024 kwenye hatua ya Hell's Gate
Kalle Rovanpera na msaidizi wake Ferm Janne wa Toyota GR Yaris wakisherehekea ushindi wa Safari Rally 2024 kwenye hatua ya Hell's Gate © WRC
Matangazo ya kibiashara

Katika mkondo ambao naibu rais wa shirikisho la kuendesha magari (FIA) barani Afrika, Rodrigo Ferreira Rocha, alikiri kuwa mgumu zaidi, ilikuwa usawa wa uangalifu wa Rovanperä wa kasi na ukomavu ambao hatimaye alipata ushindi wake wa 12 wa misururu tofauti ya WRC na ushindi wa pili wa Safari Rally.

Dereva huyo kutoka Finland akisaidiwa na Jonne Halttunen, waliongoza kwa takriban dakika moja baada ya kushinda hatua zote za Ijumaa zilizojaa miamba zinazozunguka ziwa Naivasha, kisha kujiweka katika nafasi nzuri hadi Jumamosi akifungua pengo la dakika mbili huku timu pinzani zikikabiliwa na matatizo ya kiufundi na uharibifu wa tairi.

Uongozi huo dhabiti ulimruhusu bingwa huyo mara mbili wa WRC kuendesha gari hadi kumaliza katika hatua ya mwisho ya Jumapili, ambayo ilifikia kilele huku kukiwa na mandhari nzuri eneo la Hell's Gate huku Rais wa Kenya William Ruto akihudhuria.

Dereva Takamoto Katsuta wa Toyota kwenye hatua ya Soysambu siku ya Jumamosi
Dereva Takamoto Katsuta wa Toyota kwenye hatua ya Soysambu siku ya Jumamosi © WRC

Takamoto Katstuta alikamilisha nafasi mbili za kwanza kwa timu ya Toyota Gazoo Racing Yaris huku mkali wa M-Sport Ford Puma Adrien Fourmaux kutoka Ufaransa, akiambulia jukwaa lake la pili mfululizo kwa sekunde 47.3.

"Ni hali spesheli kushinda hapa," Rovanperä alifurahi.

"Pia, tukio la hadithi kwa Toyota. Tumekuwa wazuri sana hapa na hiyo inaendelea. Kama wanavyosema hapa Afrika: gari lililo mbele daima ni Toyota!

"Shukrani kubwa kwa timu, kila mtu alifanya juhudi kubwa. Nadhani mimi na Jonne tulifanya kazi nzuri, sidhani kama unaweza kuwa na Safari Rally bora kuliko sisi. Hakuna shida, kuendesha gari kwa busara na nadhani ilikuwa juhudi nzuri.”

Elfin Evans alimaliza Ijumaa akiwania jukwaa lakini Jumamosi yenye utata ambayo ilimfanya raia huyo kutoka Wales kusimama mara mbili kubadilisha gurudumu la upande wa jukwaa, ilimaanisha kwamba alimaliza zaidi ya dakika nne nyuma kutoka kwa mwenzake Rovanperä katika nafasi ya nne kwa jumla.

Anasalia wa pili katika msimamo wa madereva nyuma ya kiongozi Thierry Neuville, ambaye alimfuata kwa karibu dakika sita katika nafasi ya tano.

Neuville sasa anaongoza Evans kwa pointi sita lakini alistahimili wiki ya taabu ndani ya gari lake aina ya Hyundai i20 N. Matatizo ya shinikizo la mafuta siku ya Jumamosi yalimgharimu Mbelgiji huyo dakika kadhaa na uharibifu wa kusimamishwa siku ya Jumapili, uliosababishwa na mwamba kwenye mstari wa mbio, ulioongeza uharibifu. Wenzake, Esapekka Lappi na Ott Tänak walizidi kuwa pabaya.

Ni wiki ambayo mtanzania Yasin Nasser akisaidiwa na Ali Katumba kwenye gari la Ford Fiesta walilazimika kuaga mashindano baada ya kubingirika kwenye bakuli la vumbi katika hatua ya saba ya Kedong 2 (kilomita 31.50) siku ya Ijumaa.

Dereva huyo mzaliwa wa Tanzania anayeishi Uganda alipoteza udhibiti wa gari lake aina ya Ford Fiesta Mark II, linalotambulika kuwa aina ya kipekee barani Afrika. 

"Uharibifu ni mkubwa," alisema Nasser kuhusu mashine yake iliyoharibika ambayo ni ya thamani ya shilingi bilioni 1 za Uganda.

Aliagiza gari hilo mnamo Novemba 2022 kutoka kwa kampuni ya uhandisi ya riadha ya Uingereza, MSport.

"Hivyo ndivyo Mungu alivyopanga. Tunaishi kupambana siku nyingine," alisema.

Nasser ambaye ambaye alikuwa ameorodheshwa nafasi ya ishirini, alikuwa tayari kuwapa wapinzani wake kwenye kitengo cha WRC2 upinzani mkali baada ya kurejea kwenye mashindano ya Safari mwaka huu.

Yasin Nasser na Ali Katumba (Ford Fiesta) kwenye eneo la kufanyia magari marekebisho
Yasin Nasser na Ali Katumba (Ford Fiesta) kwenye eneo la kufanyia magari marekebisho © Pulse Sports Uganda

Matatizo ya Lappi yalijumuisha sanduku mbili za gia zilizovunjika mashindanoni huku Ott Tänak wa Hyundai akifanikiwa kupanda hadi nafasi ya nane nyuma ya madereva wa kitengo cha pili cha WRC (WRC2) Gus Greensmith na Oliver Solberg baada ya gari lake kusimamishwa siku ya Ijumaa.

Kukamilisha orodha ya kumi bora ni ikiwemo Jourdan Serderidis akiendesha gari la Puma na nyota wa Škoda Fabia Rally2 Kajetan Kajetanowicz.

WRC itarejea kwenye barabara za lami kwa mashindano ya Croatia mwezi ujao yatakayofanyika kuanzia tarehe 18 - 21 Aprili katika mji mkuu Zagreb.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.