Pata taarifa kuu

Francis Ngannou bondia kutoka Cameroon amefiwa na mwanawe Kobe

Mwanamasumbwi Francis Ngannou, raia wa Cameroon amethibitisha kifo cha mwanawe Kobe mwenye umri wa miezi 15 katika chapisho la mtandao wa kijamii kwenye ukurasa wake wa X.

Francis Ngannou bondia kutoka nchini Cameroon amefiwa na mwanawe.
Francis Ngannou bondia kutoka nchini Cameroon amefiwa na mwanawe. AP - Gregory Payan
Matangazo ya kibiashara

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 amethibitisha kifo cha mwanawe Kobe usiku wa Jumatatu ya wiki hii.

"Ameondoka kwa mapema zaidi, lakini ameenda," Ngannou aliandika kwenye chapisho lake.

"Mtoto wangu mchanga, mshirika wangu, Kobe alikuwa na furaha, sasa analala bila uhai. Niliita jina lake kwa sauti ya juu mara kadhaa lakini hajibu." alisema bondia huyo.

Ngannou aliinuka kutoka katika maisha ya umaskini nchini Cameroon na kuwa bingwa wa uzani  wa juu wa UFC kabla ya kubadili mkondo  kutoka MMA hadi ndondi mwaka jana.

Alipambana zaidi na Tyson Fury katika mechi yake ya kwanza ya ndondi ya kulipwa nchini Saudi Arabia Oktoba mwaka jana, na kupoteza kwa uamuzi wa majaji, kabla ya kushindwa katika raundi ya pili na Anthony Joshua mwezi Machi.

Tyson Fury na Francis Ngannou kabla ya pambano lao nchini Saudi Arabia
Tyson Fury na Francis Ngannou kabla ya pambano lao nchini Saudi Arabia REUTERS - AHMED YOSRI

Mpiganaji mwenzake wa UFC Conor McGregor alikuwa miongoni mwa waliotuma ujumbe wa rambirambi kwa bondia huyo.

Kocha wa Ngannou Eric Nicksick naye pia alionyesha kusikitishwa kutokana na msiba uliompata bondia huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.