Pata taarifa kuu
SOMALIA-MAJANGA

Ukame waendelea kusababisha madhara Somalia

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa, ukame unaoendelea kushuhudiwa nchini Somalia, umewaacha watu zaidi ya Milioni 2 bila chakula, maji na maeneo ya mifugo kutopata lishe.

Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. STUART PRICE / AU-UN IST PHOTO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamo OCHA, inaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya kwa msimu wa nne mfululilizo kufuatia kushuka kwa viwango vya mvua katika katika hilo la pembe ya Afrika.

Watu wapatao Milioni 2 na Laki tatu kutoka Wilaya 57 kati ya 74 wapo katika hali mbaya kwa mujibu wa ripoti ya Umoja huo

Watu wengine zaidi ya Laki Moja wameyakimbia makwao, wakienda kutafuta chakula, maji na malisho kwa mifugo yake.

Waziri wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia Khadija Diriye anaonya kuwa watu huenda wakapoteza maisha na kuwa masikini zaidi iwapo usluhu ya hatraka haitachukuliwa.

Walio kwenye hatari kubwa ni watoto, wanawake, wazee na walemavau iwapo hawatapata msaada wa haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.