Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Mapigano katikati mwa Somalia, UN na Amisom waonya

Umoja wa Mataifa na tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM wanatoa wito wa "kukomeshwa mara moja" kwa uhasama. Mapigano katika jimbo la Galmudug yameendelea kuripotiwa kati ya vikosi vinavyounga mkono serikali na wanamgambo wa Kisufi wa Ahly Sunna Wa Jamaa kwa siku kadhaa.

Mwanajeshi wa Somalia katika kambi ya kijeshi ya Sanguuni mnamo 2018.
Mwanajeshi wa Somalia katika kambi ya kijeshi ya Sanguuni mnamo 2018. AFP - MOHAMED ABDIWAHAB
Matangazo ya kibiashara

Tayari mapigano hayo yameua watu kumi na wawili kulingana na vyanzo vya usalama. Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu hatmaya raia kufuatia mapigano haya na pia inahofia kwamba yatachelewesha zaidi mchakato unaoendelea wa uchaguzi.

Mapigano hayo tayari yamewakosesha makazi watu 100,000, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, na kufanya iwe vigumu kuwapata wahanga wa mzozo huo. Hili linatia wasiwasi zaidi kwani "hospitali mbili" "zimeathiriwa" na mapigano, Umoja wa Mataifa umelaani katika taarifa yake.

Mbali na hali ya kibinadamu, nambari 1 wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Mmarekani James Swan, anahofia kwamba mapigano haya "yatavuruga" nia ya mamlaka ya Somalia "kwa kuweka vipaumbele vyake vingine" ambavyo ni "kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi na mwendelezo wa mapambano dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabab”. Haya ndiyo aliyoyasema katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne. Alizitaka pande zinazohusika kusuluhisha mgogoro wao kwa njia ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.