Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

DRC: Kesi ya Vital Kamerhe yaahirishwa hadi Agosti 7, 2020

Mwezi mmoja baada ya kumalizika kwa kesi yake ya kwanza, Vital Kamerhe amefikishwa kwa mara nyingine mbele ya majaji leo Ijumaa Julai 24, 2020. Lakini baada ya dakika chache kufunguliwa, kesi ya mkurugenzi ofisi ya rais Tshisekedi imeahirishwa hadi Agosti 7 kwa sababu ya utaratibu.

Vital Kamerhe picha iliyopigwa Novemba 11, 2018 huko Geneva.
Vital Kamerhe picha iliyopigwa Novemba 11, 2018 huko Geneva. Fabrice COFFRINI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kesi ya leo ya Vital Kamerhe katika Mahakama ya Rufaa ilisikilizwa kwa muda mfupi.

Mawakili wa Vital Kamerhe wameendelea kuomba mteja wao aachiliwe huru, wakibaini kwamba hana hatia yoyote.

"Hakuna wizi. Hakuna ushahidi wa ufisadi, "wanasheria wa Kamerhe wamebaini. Wakati huo huo wamewasilisha ombi jipya la mteja wao kuachiliwa kwa dhamana.

Wameelezea hofu yao kuhusiana na janga la Corona ambalo wamesema kuna hatari ya wafungwa katika jela ya Makala, anakozuiliwa Vital Kamerhe, kuambukizwa virusi hivyo.

Mahakama ya mwanzo ilimuhukumu Vital Kamerhe kifungo cha miaka 20 kwa ufisadi na wizi wa takriban dola za Marekani milioni 50.

Bw. Kamerhe ni mwanasiasa maarufu katika siasa za taifa la DR Congo na ndie mtu muhimu wa muungano uliomsaidia rais Felix Tshisekedi kushinda uchaguzi na kuchukua madaraka.

Alimuunga mkono Tshisekedi katika kampeni zake za mwaka 2018 akitarajia kwamba atarejesha mkono mwaka 2023.

Vital Kamerhe ndie mwansiasa mkuu zaidi kukabiliwa na mashtaka katika taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati ambapo kuna ufisadi wa kiwango cha juu.

Kamerhe alikana kuiba fedha zilizotengewa mradi wa ujenzi wa nyumba za serikali chini ya uogozi wa rais Tshisekedi na kuyataja mashtaka hayo kuwa ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.