Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Hukumu dhidi ya Vital Kamerhe: Chama cha UNC chanyooshea kidole cha lawama majaji

Chama cha  siasa cha UNC kinachoongozwa na  Vital Kamerhe kimelaani hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela dhidi ya kiongozi wake baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi.

Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa.
Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa chama hicho wameshutumu majaji waliotoa hukumu hiyo kwa kile walichosema  hawakuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu kesi dhidi ya kionbgozi wao.

Jaji Pierrot Bakenge, aliitangaza hukumu ya kifungo cha miaka ishirini dhidi ya Vital Kamerhe kwa kesi ya ufisadi ambayo ilikuwa inamkabili. Hukumu ambayo hadi sasa chama chake wameendelea kutupiliwa mbali wakisema kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa ambayo inalenga kumtenga kiongozi wao katika siasa za DRC.

“Hatutakubali kiongozi wetu afungwe kwa vitu ambavyo hakufanya. UNC tumeelewa kwamba madai yote haya yanalenga kumpaka tope ili asiwe mgombea kwa uchaguzi wa mwaka 2023, “ alisema Sele Yemba, msemaji wa chama cha Vital kamerhe cha UNC.

Kwa upande wake Chama cha UDPS mshirika wa chama cha Kamerhe kimesema, hatua hio haiwezi kuvunja uhusiano wao.

“Chama cha UDPS tumesema kuwa, ndugu zetu wa UNC tuko pamoja, kwani ule ambae amefungwa ni bwana Kamerhe, lakini UNC iko, tutaendelea kushirikiana pamoja, UDPS na UNC ni muungao mmoja, “ alisema Adolphe Amisi, msemaji wa chama cha UDPS cha raïs Felix Tshisekedi.

Vital Kamerhe anashtumiwa kutumia vibaya zaidi ya dola milioni 50 za Marekani zilizokuwa zimetengwa kugharamia ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa.

Mawakili wake wamesema watakata rufaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.