Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Kifungo cha miaka ishirini dhidi ya Vital kamerhe chaibua maoni tofauti DRC

Nchini DRC, maoni  yametofautiana kuhusu kifungo cha miaka 20 jela alichopewa mwanasiasa Vital Kamerhe na Mahakama ya jijini Kinshasa mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji huo mkuu baada ya kupatikana na makosa ya kufuja fedha za umma.

Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa.
Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Hali kama hiyo pia imeshuhudiwa mjini Bukavu na katika maeneo mengi ya mkoa Kivu Kusini, ambako Vital Kamerhe anatokea.

Vital Kamerhe anashtumiwa kutumia vibaya zaidi ya dola milioni 50 za Kimarekani zilizokuwa zimetengwa kugharamia ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa.

Kamerhe alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya rais, kabla ya kuakamatwa kwake na kushtakiwa.

Jaji Pierrot Bakenge, aliitangaza hukumu ya kifungo cha miaka ishirini dhidi ya Vital Kamerhe kwa kesi ya ufisadi ambayo ilikuwa inamkabili. Hukumu ambayo hadi sasa chama chake wameendelea kutupiliwa mbali wakisema kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa ambayo inalenga kumtenga kiongozi wao katika siasa za DRC.

“Hatutakubali kiongozi wetu afungwe kwa vitu ambavyo hakufanya. UNC tumeelewa kwamba madai yote haya yanalenga kumpaka tope ili asiwe mgombea kwa uchaguzi wa mwaka 2023, “ amesema Sele Yemba, msemaji wa chama cha Vital kamrehe cha UNC.

Hata hivyo Chama cha UDPS mshirika wa chama cha Kamerhe kimesema, hatua hio haiwezi kuvunja uhusiano wao.

 “Chama cha UDPS tumesema kuwa, ndugu zetu wa UNC tuko pamoja, kwani ule ambae amefungwa ni bwana Kamerhe lakini UNC iko, tutaebdelea kushirikiana pamoja, UDPS na UNC ni muungao mmoja, “ Adolphe Amisi, msemaji wa chama cha UDPS cha raïs Felix Tshisekedi.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya DRC kuona afisa mwandamizi akihukumiwa na kufungwa jela akiwa anatekeleza majukumu yake serikalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.