Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

DRC: Mashirika ya kiraia yagawanyika juu ya kesi ya Vital Kamerhe

Vital Kamerhe, mnadhimu wa zamani wa ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 kwa madai ya kutumia vibaya zaidi ya dola milioni 50 za Kimarekani zilizokuwa zimetengwa kugharamia ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa.

Vital Kamerhe, Novemba 11, 2018 huko Geneva.
Vital Kamerhe, Novemba 11, 2018 huko Geneva. Fabrice COFFRINI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kesi yake katika mahakama ya Gombe kumalizika siku ya Alhamisi, majaji wanatarajia kutoa uamuzi wao Juni 20.

Kwa upande wa mashirika mengi ya kiraia yanayopambana dhidi ya ubadhirifu wa mali ya umma, yanasema kesi hii angalau ingekuwa na sifa ya kuonyesha ukweli kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.

Moja ya mashirika hayo limeendelea kukosoa usimamizi wa mpango wa dharura wa siku 100.

Nalo shirika la ODEP, limebaini kwamba tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa ilionekana dhahiri kwamba kulikuepo na ukiukwaji wa sheria na sera za fedha za umma na hakukuwepo udhibiti kamili. Na wale ambao walihusika kwa madai hayo matumizi mabaya ya fedha hizo pia walitakiwa kuwa upande wa washtakiwa.

"Pia ni ukiukwaji huu wa sheria unaosababisha matumizi haya mabaya," amesema Valery Madianga, afisa wa mawasiliano katika shirika la ODEP. Kwa sababu ingelikuwa sheria iliheshimishwa, na kwamba Waziri wa Bajeti, wa Fedha, walitekeleza majukumu yao ipasavyo, nadhani kile kilichotokea leo kingeliweza kuepukika.

Mashirika mengine kadhaa yamelaani hoja ya mwendesha mashitaka ambaye alimhusisha Vital kamerhe kwa kosa la msichana wake au mwipa wake baada ya kupokea hongo kutoka kwa Jammal amabye pia anashtumiwa katika kesi hiyo.

Upande wa mashtaka unataka Kamerhe ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela, pamoja na kunyang'anywa mali zake anazodaiwa kuwa zilipatikana kwa fedha za umma.

Hata hivyo wanasheria wake wameomba mteja wao aachiliwe huru, wakibaini kwamba hana hatia yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.