Pata taarifa kuu
DRC-UN-MONUSCO-USALAMA

Umoja wa Mataifa wapiga kura ya kupunguza idadi ya askari wa MONUSCO DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, kuendelea na shughuli zake nchini humo.

Magari ya Monusco jijini Kinshasa (picha ya kumbukumbu).
Magari ya Monusco jijini Kinshasa (picha ya kumbukumbu). © REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo llimechukuliwa kutokana na hatua kubwa ambayo imepigwa hivi karibuni nchini DRC, na idadi ya askari wa kikosi cha MONUSCO imepunguzwa na kuongezwa idadi ya maafisa wa polisi, ili kukabiliana na hali inayoendelea nchini DRC, hasa mashariki mwa nchi hiyo.

Ufaransa iliwasilisha azimio hilo ambalo pia limependekeza kuwa, idadi ya wanajeshi ipunguzwe lakini idadi ya polisi iongezwe, wakati huu wakaazi wa Wilaya ya Beni na maeneo mengine wakiendelea kushambuliwa na makundi ya waasi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limebaini kwamba lina imani na MONUSCO, licha ya uamuzi huo wa kupinguza idadi ya askari wake.

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya kushuhudiwa mfululizo wa mashambulizi ya waasi wa Uganda, ADF, yaliyogharimu maisha ya watu wengi, mashariki mwa DRC, hususan katika eneo la Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kwa miaka miwili maeneo kadhaa yaliwekwa chini ya himaya ya jeshi la serikali kutoka mikononi mwa makundi ya waasi, kwa mujibu wa wanadiplomasia, huku waibaini kwamba maafisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa watakuwa na kazi kubwa ya kulinda raia.

Azimio hilo limeungwa mkono na wajumbe wote wa Baraza hilo, wakati huu makundi ya waasi hasa katika Wilaya ya Beni yakiendelea kushambulia na kuua raia, ambao wanalishtmu jeshi la Monusco kwa kushinwa kuwalinda na wamekuwa wakiandamana wakitaka jeshi hilo kuondoka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.