Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-UN-MONUSCO

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix atembelea Beni

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amekuwa akitembelea mji wa Beni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo limeshuhudia mauaji ya zaidi ya watu 100 tangu tarehe 5 mwezi Novemba, mauaji ambayo yametekelezwa na waasi wa ADF Nalu.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Jean-Pierre Lacroix  akiwa mjini Beni Novemba 30 2019
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix akiwa mjini Beni Novemba 30 2019 Flickr/Monusco
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ambayo imekuja, wakati wakaazi wa Beni wakiwa na hasira na jeshi la Umoja wa Mataifa, na wiki hii wameandamana mjini Beni, Goma na jiji kuu Kinshasa, kulishtumu jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa kushindwa kuwalinda raia.

Lacroix ametembelea kambi ya MONUSCO ambayo ilivamiwa na waandamanaji wenye hasira, lakini pia amekuwa akikutana na wakuu wa jeshi la DRC.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa anayehusika na operesheni za kulinda amani, amezuru Mashariki mwa nchi hiyo baada ya rais Felix Tshisekedi kukutana na uongozi wa Monusco kuwa, kutakuwa na operesheni ya pamoja dhidi ya makundi ya waasi.

Wakati uo huo, mashirika ya kiraia yakiongozwa na CEPHADO, yamelaani mauaji dhidi ya raia, Wilayani Beni na kutaka juhudi zaidi kufanyika kuwalinda raia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.