Pata taarifa kuu
DRC-BENI-USALAMA

DRC: Miili kumi na tisa yapatikana Beni

Miili kumi na tisa imepatikana Jumatano, Novemba 27 katika eneo la Maleki, karibu kilomita kumi kutoka mji wa Oicha, katika Wilaya ya Beni, kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na vyanzo vya Umoja wa Mataifa.

Askari wa kikosi cha Umoja w Mataifa nchini DRC (MONUSCO), Aprili 11, 2019, katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo makundi kadhaa ya silaha yanaendelea kuhatarisha usalama.
Askari wa kikosi cha Umoja w Mataifa nchini DRC (MONUSCO), Aprili 11, 2019, katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo makundi kadhaa ya silaha yanaendelea kuhatarisha usalama. © ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wahanga waliuawa kwa mapanga na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda wa ADF. Mauaji haya yanatokea mbili baada ya maandamano makubwa dhidi ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, maandamano yaliyokumbwa na vurugu na kusababisha vifo wilayani Beni.

Shambulio hilo lilitokea kama kilomita 10 kutoka kambi ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa. Ripoti ya kwanza iliyotolewa na asasi za kiraia ilibaini kwamba watu 14 waliuawa saa kumi na mbili asubuhi. Sasa idadi hiyo imeongezeka hadi 19.

Wilaya ya Beni imeendelea kukumbwa na zimwi la mauaji, huku raia wakiendelea kulalamikia usalama wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.