Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Chanjo ya pili dhidi ya virusi vya Ebola yaanza kutolewa Goma

Maafisa wakuu wa afya nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameanza kutoa chanjo ya pili ya ugonjwa wa Ebola iliyotengezwa na kampuni ya Johnson and Johnson kukabiliana na virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo.

Operesheni ya kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola, Goma mnamo Agosti 7, 2019.
Operesheni ya kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola, Goma mnamo Agosti 7, 2019. Augustin WAMENYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mratibu wa mpango wa kupambana na Ebola nchini humo Dokta Jean-Jacques Muyembe, amesema kuwa kuna hatua sita muhimu zinazofuatwa wakati wa kupewa chanjo hiyo, kwa lengo la kujiridhisha.

Chanjo hii inatolewa mara mbili kw watu, ambapo siku 58 zinahesabiwa baada ya kupewa chanjo ya kwanza, amesema Patient Kighoma, mkurugenzi wa idara ya afya inayohusika na masuala ya chanjo katika shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka, MSF, mjini Goma.

Katika taarifa, taasisi ya afya ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa chanjo hiyo ya pili iliyotengezwa na kampuni ya Johnson and Johnson itaanza kutumiwa katika maeneo ambayo ugonjwa huo wa Ebola hauenei kwa haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.