Pata taarifa kuu

Marekani: Meli ya mizigo iliyozamishwa na shambulio la Houthi inahatarisha mazingira

Jeshi la Marekani limeonya siku ya Jumapili, Machi 3, juu ya hatari kwa mazingira baada ya kuzama kwa Rubymar Jumamosi hii. Meli hiyo ilizamishwa na waasi wa Houthi wa Yemen, ilikuwa imesheheni mbolea zinazoweza kuwaka.

Picha ya setilaiti inaonyesha meli ya mizigo yenye bendera ya Belize, inayomilikiwa na Uingereza ya Rubymar kabla ya kuzama kwenye Bahari Nyekundu mnamo Machi 1, 2024.
Picha ya setilaiti inaonyesha meli ya mizigo yenye bendera ya Belize, inayomilikiwa na Uingereza ya Rubymar kabla ya kuzama kwenye Bahari Nyekundu mnamo Machi 1, 2024. © Maxar technologies / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rubymar, meli ya biashara yenye bendera ya Belize inayotumiwa na kampuni ya Lebanon, hatimaye ilizama siku ya Jumamosi, Machi 2, katika Bahari Nyekundu, nje ya pwani ya Yemen. Ilikuwa ikisafiri kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na bandari ya Bulgaria ya Varna. Inatoa hatari kwa mazingira, jesi la Marekani lilionya - siku hiyo.

Tangu Novemba mwaka jana, Wahouthi wamefanya mashambulizi dhidi ya meli katika Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden, wakisema wanafanya hivyo kwa mshikamano na Wapalestina huko Gaza. Kwa mujibu wa Kamandi Kuu ya Marekani, meli hiyo ilipigwa na makombora mawili yabalistiki mwezi uliopita. Waasi wa Houthi walidai kuhusika na shambulio hilo. Ingawa wafanyakazi waliweza kuhamishwa hadi mahali salama, mizigo ilibaki: tani 21,000 za mbolea.

Hatari kubwa ya uchafuzi wa mazingira

Zinapooza, mbolea hizi zinaweza kutoa gesi zenye sumu. Pia hutoa molekuli hatari ndani ya maji, ikiwa ni pamoja na sulfuri au asidi. Athari zao kwa mazingira na afya zinatambuliwa. Kwa hiyo zinawasilisha "hatari kwa mazingira katika Bahari ya Shamu", linaonya jeshi la Marekani katika taarifa kwa vyombo vya habari. Picha za satelaiti pia zinaonyesha kuwa mafuta yanavuja kutoka kwenye mabaki.

Marekani pia inabaini kwamba kwa kuzama, meli hiyo inatoa hatari ya athari, chini ya uso, kwa meli nyingine zinazotumia njia hii maarufu. Mashirika mengine kadhaa pia yameelezea wasiwasi wao kuhusu tishio la mazingira linaloletwa na meli hiyo ya mafuta.

Picha za satelaiti zilizoshirikiwa na Maxar Technologies na kuchapishwa na shirika la habari la AFP zinaonyesha mafuta yakitoka kwenye meli. Kulingana na tovuti ya TankerTrackers, kuzama huko "kutasababisha maafa ya kimazingira katika maji ya eneo la Yemeni na Bahari Nyekundu".

Usafirishaji wa makontena katika Bahari Nyekundu umepungua kwa karibu theluthi moja mwaka huu, kulingana na Shirika la Fedha la Kimataifa, kutokana na kuendelea kwa mashambulizi ya waasi wa Houthi wa Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.