Pata taarifa kuu

Houthi: Mashambilizi ya Marekani na Uingereza hayatobakia hivo 'bila kujibiwa'

Mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen na Marekani na Uingereza hayatobakia hivo "bila kujibiwa", waasi hao wa Yemen wametishia katika taarifa yao siku ya Jumanne, wakionyesha kwamba mashambulizi 18 yalilenga eneo nchi yao. 

Katika picha hii iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, ndege ya jeshi la Wanahewa FGR4 inapaa na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya wanajeshi wa Houthi nchini Yemen, kutoka RAF Akrotiri, Cyprus, Jumatatu, Jan. Tarehe 22, 2024. Wanajeshi wa Marekani na Uingereza walishambulia kwa mabomu maeneo manane yanayotumiwa na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen Jumatatu usiku, ikiwa ni mara ya pili kwa washirika hao wawili kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa safu ya uwezo wa waasi hao.
Katika picha hii iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, ndege ya jeshi la Wanahewa FGR4 inapaa na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya wanajeshi wa Houthi nchini Yemen, kutoka RAF Akrotiri, Cyprus, Jumatatu, Jan. Tarehe 22, 2024. Wanajeshi wa Marekani na Uingereza walishambulia kwa mabomu maeneo manane yanayotumiwa na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen Jumatatu usiku, ikiwa ni mara ya pili kwa washirika hao wawili kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa safu ya uwezo wa waasi hao. AP - AS1 Jake Green RAF
Matangazo ya kibiashara

 

"Mashambulizi haya hayatobakia hivo bila kujibiwa na bila kuadhibiwa," amesema msemaji wa jeshi la Houthi Yahya Saree katika chapisho kwenye mtandao wa X, akibaini kwamba mashambulizi yalilenga mikoa ya Sanaa, Hodeida, Taez na Al-Bayda.

Mashambulio ya hivi punde ya Marerkani na Uingereza, yalilenga maeneo  ya Houthi nchini Yemen, kutokana na mashambulio ya Houthi dhidi ya meli za kimataifa na kibiashara, na yananuia kudhoofisha uwezo wa waasi hao unaotishia biashara ya kimataifa.

Hata hivyo waasi wa Houthi wameapa kuendelea na mashambulio yao, katika moja ya mzozo, unaohusishwa na vita vya Israel na Hamas ambavyo vimeongeza hali ya wasiwasi katika eneo la mashariki ya kati.

Mapema jumatau, waasi wa Houthi walidai kuishambulia meli ya mizigo ya Marekani pwani ya Yemen, msemaji wao yahya Saree akisema waliongoza oparesheni ya kijeshi kulenga meli ya mizigo ya kijeshi ya Marekani karibu na bahari nyekundu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.