Pata taarifa kuu

Bahari Nyekundu: Waasi wa Houthi wafanya shambulio jdhidi ya meli ya Marekani

Waasi wa Houthi kutoka Yemen wamedai kuhusika mapema Ijumaa, Januari 19, kwa shambulio dhidi ya meli ya wafanyabiashara kutoka Marekani iliyokuwa ikisafiri katika Ghuba ya Aden. Mashambulizi haya ni sehemu ya wiki ambayo imeshuhudia kuongezeka kwa mvutano na majibu ya Uingereza na Marekani, yaliyofanywa chini ya bendera ya muungano wa kimataifa ulioanzishwa na Washington kulinda usafiri katika ukanda huu wa bahari muhimu kwa biashara ya kimataifa.

Destroyer USS Laboona, meli kubwa ya Jeshi la wanamaji la Marekani, Desemba 25, 2023 katika Bahari Nyekundu.
Destroyer USS Laboona, meli kubwa ya Jeshi la wanamaji la Marekani, Desemba 25, 2023 katika Bahari Nyekundu. AFP - ELEXIA MORELOS
Matangazo ya kibiashara

 

"Vikosi vya wanamaji vya jeshi la Yemen (jina linalopewa tawi la kijeshi la Houthi) wamefanya operesheni ya kushtukiza dhidi ya meli ya Marekani, Chem Ranger, katika Ghuba ya Aden kwa kurusha makombora kadhaa, baadhi ya makombora yalipiga meli hiyo,” waasi wa Houthi wamesema kwenye taarifa.

Kamandi ya jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati (Centcom) imethibitisha kwamba Houthis walifanya shambulio dhidi ya meli ya wafanyabiashara, Chem Ranger, lakini kwa "makombora mawili",  bila hata hivyo kuifikia kama waasi wanavyodai. Kwa mujibu wa tovuti maalum ya Marine Traffic, Chem Ranger ni meli ya Marekani inayopeperusha bendera ya Visiwa vya Marshall ambayo imekuwa nje ya pwani ya Yemen katika siku za hivi karibuni.

Wahouthi wanasema wanazishikilia meli za China na Urusi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema China imetoa wito wa kukomesha unyanyasaji wa meli za kiraia kwenye "njia hii muhimu ya biashara ya kimataifa kwa bidhaa na nishati." "Tunatoa wito wa kukomeshwa kwa unyanyasaji wa meli za kiraia na kuendeleza mashambulizi dhidi ya meli za biashara," amesema katika mkutano na waandishi wa habari wakila siku. Beijing inajaribu kudumisha kutoegemea upande wowote katika vita vya Gaza, madhara ambayo yanaathiri eneo zima. Hivyo, China haishiriki katika muungano wa kimataifa chini ya bendera ya Marekani katika Bahari Nyekundu. Lakini hatari za kiuchumi ni kubwa na zinaweza kushinikiza China kubadili msimamo, hasa dhidi ya mshirika wake Iran, katika kujaribu kupunguza mvutano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.