Pata taarifa kuu

Marekani yadungua kombora lililorushwa kutoka Yemen dhidi ya meli kubwa ya Marekani

Vita kati ya Israel na kundi la Hamas kutoka Palestina ilipita kizingiti cha siku 100 Jumapili Januari 14. Huko Gaza, vita bado vinaendelea na huko Israeli ndugu wa mateka bado wanaishi kwa wasiwasi juu ya hatima yao.

Ndege ya Marekani ikipaa kutoka eneo lisilojulikana ili kujiunga na operesheni ya muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya Houthi nchini Yemen, Januari 12, 2024.
Ndege ya Marekani ikipaa kutoka eneo lisilojulikana ili kujiunga na operesheni ya muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya Houthi nchini Yemen, Januari 12, 2024. via REUTERS - US CENTRAL COMMAND VIA X
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Ndege ya kivita ya Marekani ilidungua kombora lililorushwa kutoka eneo linalodhibitiwa na Wahouthi huko Yemen dhidi ya meli kubwa ya Marekanik katika Bahari Nyekundu. Hakuna majeraha au uharibifu ulioripotiwa.

■ Kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, alizungumza Jumapili hii, Januari 14, wiki moja baada ya kuuawa kwa kamanda wa Hezbollah, Wissam al-Tawil. Alisema kwamba "uchokozi wa Marekani katika Bahari Nyekundu utadhoofisha uhuru wa usafiri katika bahari hiyo." Pia alidai kuwa Hezbollah iko tayari kwa vita vya pande zote.

■ Waisraeli walionyesha mshikamano siku ya Jumapili na mateka walioshikiliwa katika eneo la Palestina kuadhimisha siku 100 za kushikiliwa kwao na kuunga mkono uhamasishaji wa familia zao. Lakini msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas, Abou Obeida, alisema kwamba mateka wengi "huenda waliuawa hivi karibuni", wengine wako "katika hatari kubwa", kuihusisha Israeli kwa mauaji ya mateka hao.

■ Kulingana na ripoti iliyotangazwa Jumapili hii, Januari 14 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 23,968 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Zaidi ya 60,000 walijeruhiwa. Zaidi ya watoto 10,000 - au 1% ya jumla ya watoto katika Ukanda wa Gaza - wameuawa, kulingana na ripoti mpya kutoka shirika la Save The Children.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.