Pata taarifa kuu

Urusi yaitisha mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Urusi imeomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani na Uingereza nchini Yemen, ujumbe wa kudumu wa Urusi katika Umoja wa Mataifa umeliambia shirika la habari la REUTERS. 

Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York.
Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York. AP Photo/Mary Altaffer, File
Matangazo ya kibiashara

Marekani na Uingereza zimeanzisha mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya maeneo ya kijeshi ya wasi wa Houthi nchini Yemen, katika kile ambacho kimeelezwa kuwa ni upanuzi mkubwa wa kikanda wa vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza.

Iran yalaani mashambulizi ya Marekani na Uingereza yanayolenga waasi wa Houthi nchini Yemen

Iran imelaani Ijumaa hii mashambulizi ya anga yaliyofanywa usiku kucha na Marekani na Uingereza dhidi ya malengo ya waasi wa Houthi nchini Yemen, ikisema ni "hatua ya kiholela" na "ukiukaji wa wazi wa uhuru" wa nchi hii. Katika taarifa yake, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kanani, "amelaani vikali mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani na Uingereza dhidi ya miji kadhaa nchini Yemen", baada ya kuongezeka kwa mashambulizi ya waasi wanaoungwa mkono na Iran kushambulia meli katika Bahari ya Shamu.

Wahouthi kuendelea kulenga meli zinazohusishwa na Israeli katika Bahari Nyekundu

Msemaji wa waasi nchini Yemen, Mohamed Abdel Salam, amesema Ijumaa kwamba Wahouthi wataendelea kulenga meli zenye uhusiano na Israel katika Bahari Nyekundu, na kulaani mashambulizi "yasiyo ya haki" ya Marekani na Uingereza dhidi ya kundi lake. "Hakuna uhalali wa uvamizi huu dhidi ya Yemen, kwani hakukuwa na tishio kwa urambazaji wa kimataifa katika Bahari Nyekundu (...), na mashambulizi yalikuwa na yataendelea kulenga meli za Israeli au zile zinazoelekea kwenye bandari za Palestina inayokaliwa kwa mabavu," ameandika kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Maandamano mjini New York dhidi ya mashambulizi ya Marekani nchini Yemen

Waandamanaji wanaopinga vita wamekusanyika mjini New York kupinga mashambulizi ya Marekani na Uingereza nchini Yemen. Video zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha waandamanaji wakikusanyika katika uwanja wa Times Square wakiwa na mabango ya kutaka kusitishwa kwa hatua ya Israel kukalia maeneo ya Palestina na Marekani kusitisha mashambulizi yake nchini Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.