Pata taarifa kuu

Waasi wa Huthi wanadai kushambulia meli ya Marekani

Waasi wa Yemen wamesema siku ya Jumatano wamerusha "ndege zisizo na rubani na makombora" dhidi ya meli ya Marekani, baada ya vikosi vya Uingereza na Marekani kusema vimezuia "shambulio kubwa zaidi" la waasi Wahuthi katika Bahari ya Shamu.

Wapiganaji wapya walioajiriwa, waliojiunga na kikosi cha kijeshi cha Houthi kilichonuiwa kutumwa vitani kusaidia Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, wakiandamana katika gwaride mjini Sanaa, Yemen, Desemba 2, 2023.
Wapiganaji wapya walioajiriwa, waliojiunga na kikosi cha kijeshi cha Houthi kilichonuiwa kutumwa vitani kusaidia Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, wakiandamana katika gwaride mjini Sanaa, Yemen, Desemba 2, 2023. REUTERS - KHALED ABDULLAH
Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wenye uhusiano na Iran, wamefanya "operesheni (...) yenye idadi kubwa ya makombora, balestiki na majini, na ndege zisizo na rubani wakilenga meli ya Marekani iliyokuwa ikitoa msaada kwa taasisi ya Kizayuni", walitangaza katika taarifa, bila kutaja tarehe au eneo la shambulio hilo. Hili ni "jibu la kwanza kwa shambulio la hila dhidi ya vikosi vyetu mnamo Desemba 31," wameongeza. Zikijibu ombi la usaidizi kutoka kwa meli ya kibiashara, helikopta za Jeshi la Wanamaji la Marekani zilizamisha boti tatu za waasi wa Huthi siku hiyo, na kuua wafanyakazi kumi.

Tangu kuanza kwa vita Oktoba 7 kati ya Israel na Hamas, Wahuthi wanaodhibiti sehemu kubwa ya Yemen, wameongeza mashambulizi katika Bahari Nyekundu dhidi ya meli zinazoshukiwa kuwa na uhusiano na Israel, wakidai kufanya kazi kwa mshikamano na Wapalestina kutoka Gaza.

Ili kuepuka Bahari Nyekundu, kwa sababu ya vitisho kutoka kwa waasi wa Huthi, meli za wafanyabiashara zinalazimika kuzunguka Afrika.
Ili kuepuka Bahari Nyekundu, kwa sababu ya vitisho kutoka kwa waasi wa Huthi, meli za wafanyabiashara zinalazimika kuzunguka Afrika. © France 24

Mshirika wa kwanza wa Israel, Marekani, ilianzisha muungano wa kimataifa mwezi Desemba ili kupata eneo hili la kimkakati ambapo asilimia 12 ya biashara ya dunia inapita. Siku ya Jumatano, majeshi ya Uingereza na Marekani yalidai kuangusha ndege 18 zisizo na rubani na makombora matatu katika Bahari Nyekundu usiku kucha kama sehemu ya shambulio "tata".

Meli ya Uingereza ya HMS Diamond pamoja na meli za kivita za Marekani "zilifanikiwa kuzima shambulio kubwa zaidi lililofanywa hadi leo katika Bahari Nyekundu na Wahuthi", aliandika Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Grant Shapps, kwenye mtandao wa kijamii "The Diamond ilizuia mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubani kwa mwelekeo wake na ule wa meli za biashara katika eneo hilo,” aliongeza, akibainisha kuwa hakukuwa na majeruhi wala uharibifu.

Shambulio la Jumanne usiku lilikuwa la 26 dhidi ya meli katika Bahari Nyekundu tangu katikati ya mwezi wa Januari, kulingana na Kamandi ya Marekani huko Mashariki ya Kati (Centcom).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.