Pata taarifa kuu

Ukanda wa Gaza: Licha ya ahadi, mashambulizi ya anga yaongezeka

Mashambulio ya anga ya Israel kusini na katikati mwa Ukanda wa Gaza yameongezeka leo, licha ya ahadi iliyotolewa na Israel, hasa kwa mshirika wake wa Marekani, kuelekea kampeni inayolengwa zaidi ya kuwaokoa raia na kuondoa sehemu ya wanajeshi wake kutoka Palestina. Pamoja na Mahmoud Abbas siku ya Jumatano , Januari 10, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani "amethibitisha tena kwamba Marekani inaunga mkono hatua zinazoonekana za kuundwa kwa taifa la Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas mjini Ramallah Jumatano hii, Januari 10, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas mjini Ramallah Jumatano hii, Januari 10, 2024. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu

■ Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekuwa katika ziara ya kikanda tangu siku ya Jumatatu. Huko Tel Aviv siku ya Jumanne, alinuia kuishinikiza Israel kufanya zaidi kuwalinda raia katika Ukanda wa Gaza na kujaribu kukomesha ongezeko la la uhasama katika kanda hiyo. Amewaambia viongozi wa Israel kwamba kuhalalisha uhusiano na nchi za kikanda bado kunawezekana licha ya vita katika eneo hilo, lakini ikiwa tu Israeli itaunda mazingira ya kuunda taifa la Palestina linaloweza kujitegemea.

■ Mkuu wa diplomasia ya Marekani alikutana na Mahmoud Abbas siku ya Jumatano mjini Ramallah hasa kushughulikia suala lenye utata la baada ya vita huko Gaza, eneo lililoharibiwa na mashambulizi ya Israel. Antony Blinken "alithibitisha tena kwamba Marekani inaunga mkono hatua zinazoonekana kuelekea kuundwa kwa taifa la Palestina." Kisha akasafiri kwenda Bahrain.

■ Mashambulio ya anga ya Israel kusini na katikati mwa Ukanda wa Gaza yaliongezeka siku ya Jumatano hii licha ya ahadi ya Israel ya kuelekea kwenye kampeni inayolengwa zaidi ya kuwahifadhi raia na kuwaondoa baadhi ya wanajeshi wake katika eneo la Palestina.

■ Rais wa Palestina alisema kwamba "Gaza ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya taifa la Palestina, na hatutaruhusu jaribio lolote la kuwang'oa watu wetu katika Ukingo wa Magharibi, Jerusalem na Ukanda wa Gaza," aliongeza.

■ Kulingana na ripoti mpya iliyotangazwa Jumatatu Januari 8 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 23,357 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu karibu 60,000 walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.