Pata taarifa kuu

Vita inaingia mwezi wake wa 4, Antony Blinken katika Mashariki ya Kati ili kuepusha mgogoro

Wakati vita dhidi ya Hamas vikiingia mwezi wake wa nne Jumapili hii, Januari 7, Israel inadai "kuvunja" "muundo wa kijeshi" wa Hamas kaskazini mwa Gaza.

Moshi unafuka katikati mwa Gaza, Jumamosi Januari 6, 2024.
Moshi unafuka katikati mwa Gaza, Jumamosi Januari 6, 2024. REUTERS - AMIR COHEN
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Jeshi la Israel lilitangaza Jumamosi jioni kwamba "limekamilisha kuvunja muundo wa kijeshi wa Hamas kaskazini mwa Ukanda wa Gaza" na sasa lilikuwa likizingatia kusambaratisha kundi la Hamas "katikati na kusini mwa eneo hili". .

■ Mapema Jumapili, mashahidi waliripoti mashambulizi ya anga ya Israel huko Khan Younes, mji mkuu kusini mwa Ukanda wa Gaza na kitovu kipya cha mapigano hayo. Katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, uvamizi wa Israel ulisababisha vifo vya watu sita siku ya Jumapili huko Jenin, ngome ya makundi ya Wapalestina.

■ Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaendelea na ziara yake ya Mashariki ya Kati kupitia Jordan, baada ya kukutana na rais wa Uturuki siku ya Jumamosi mjini Istanbul, kwa matumaini ya kukabiliana na kusamba kwa mapigano hayo katika ukanda huo.

■ Kulingana na ripoti mpya iliyotangazwa Jumamosi Januari 6 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 22,722 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu wengine karibu 60,000 walijeruhiwa. Siku ya Alhamisi jeshi la Israel lilisema kuwa liliwaua zaidi ya wapiganaji 8,000 wa Kipalestina tangu shambulio la Oktoba 7. Wanajeshi 175 wa Israel wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza Oktoba 27, kulingana na takwimu za hivi punde za jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.