Pata taarifa kuu

Mauaji ya Kimbari Gaza: Washington yakosoa kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel mbele ya ICJ

Ikulu ya White House imekosoa ombi lililowasilishwa mbele ya Mahakama ya kimataifa na Afrika Kusini dhidi ya Israel, kwa "mauaji ya halaiki" katika Ukanda wa Gaza. "Ombi hili halina msingi, halina tija na halina ukweli wowote," amesema msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la White House John Kirby.

Kesi ikisikilizwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ). Afrika Kusini nayo imewasilisha kesi dhidi ya Israel kwenye mahakama hii ikitaka haki kutendeke.
Kesi ikisikilizwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ). Afrika Kusini nayo imewasilisha kesi dhidi ya Israel kwenye mahakama hii ikitaka haki kutendeke. UN Photo ICJ-CIJ/Frank Van Book (United Nations)
Matangazo ya kibiashara

"Hatufikirii kuwa hii ni hatua yenye tija kwa wakati huu," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller alipoulizwa kuhusu hili wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Alikataa madai yaliyotolewa dhidi ya Israel, nchi ambayo Marekani ni mshirika wa kwanza na msaidizi mkuu wa kijeshi.

Marekani "katika hatua hii haijaona vitendo vyovyote vinavyojumuisha mauaji ya halaiki" katika vita vilivyoanzishwa na Israel dhidi ya Hamas kutoka Palestina, Bw. Miller amebainisha. Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), mahakama ya juu kabisa ya Umoja wa Mataifa, itafanya vikao vyake vya kwanza vya hadhara wiki ijayo katika kesi iliyoanzishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel.

Afrika Kusini inataka ICJ kuamuru haraka kusitishwa kwa operesheni za kijeshi huko Gaza, kwa kuzingatia kwamba Israeli "imejihusisha, inashiriki na inahatarisha kuendelea na vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina huko Gaza," kulingana na mamlaka.

Marekani ilisema "haioni kitendo chochote kinachojumuisha mauaji ya kimbari" huko Gaza, ikirejelea kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki, baada ya kuishutumu serikali ya Kiyahudi kwa vitendo vya "mauaji ya halaiki".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.