Pata taarifa kuu

Israel yakanusha tuhuma za mauaji ya halaiki ya Afrika Kusini katika ICJ

Israel imekanusha "kwa kuchukizwa" na tuhuma za "vitendo vya mauaji ya halaiki" katika vita vyake huko Gaza vilivyoletwa dhidi yake na Afrika Kusini mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel imesema.

Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko Hague nchini Uholanzi.
Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko Hague nchini Uholanzi. AP - Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

"Israel inakataa kwa kuchukizwa na kashfa ya damu inayoenezwa na Afrika Kusini na matumizi yake kwa ICJ.

Mkuu wa WHO 'atiwa wasiwasi' na tishio la magonjwa ya kuambukiza huko Gaza

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema siku ya Ijumaa kwamba "ana wasiwasi sana" na tishio linaloongezeka la magonjwa ya kuambukiza katika Ukanda wa Gaza.

"Wakati idadi ya watu wanaendelea kuhama kwa kiasi kikubwa katika Kusini mwa Ukanda wa Gaza, huku baadhi ya familia zikilazimika kuhama mara nyingi na nyingi zikikimbilia katika vituo vya afya vilivyojaa watu, mimi na wenzangu wa WHO- Tunasalia na wasiwasi mkubwa kuhusu tishio linaloongezeka la magonjwa ya kuambukiza," Tedros amesema kwenye X, zamani ikiitwa Twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.