Pata taarifa kuu

Mauaji ya halaiki dhidi ya Israeli: Afrika Kusini yaapa kutetea Palestina mbele ya ICJ

Kwa kuikabili Israel, ambayo inaishutumu kwa "vitendo vya mauaji ya halaiki" huko Gaza, mbele ya mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi, serikali ya Afrika Kusini inatarajia kujitokeza katika anga za kimataifa na kupata umaarufu nyumbani kabla ya uchaguzi hatari kwa chama chake.

Nafasi ya Pretoria inayounga mkono Palestina imeonyeshwa mara kadhaa. Hapa, Rais wa Afrika Kusini na mwenyekiti wa African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa akiwa amevalia keffiyeh ya Palestina (katikati), Moulana Ebrahim Bham (kushoto) na Moulana Abudul Khaliq Allie (kulia), wote wajumbe wa Baraza la Umoja wa Maulamaa wa Afrika Kusini (UUCSA), wakihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kati ya UUCSA na Marafiki wa Palestina wa Afrika Kusini katika Nyumba ya Chief Albert Luthuli huko Johannesburg mnamo Desemba 18, 2023.
Nafasi ya Pretoria inayounga mkono Palestina imeonyeshwa mara kadhaa. Hapa, Rais wa Afrika Kusini na mwenyekiti wa African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa akiwa amevalia keffiyeh ya Palestina (katikati), Moulana Ebrahim Bham (kushoto) na Moulana Abudul Khaliq Allie (kulia), wote wajumbe wa Baraza la Umoja wa Maulamaa wa Afrika Kusini (UUCSA), wakihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kati ya UUCSA na Marafiki wa Palestina wa Afrika Kusini katika Nyumba ya Chief Albert Luthuli huko Johannesburg mnamo Desemba 18, 2023. © Roberta Ciuccio / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ombi la  malalamiko lenye kurasa 84 kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) huko Hague, Afrika Kusini inawataka majaji kuamuru haraka Israel "kusimamisha mara moja operesheni zake za kijeshi" katika Ukanda wa Gaza.

Pretoria inaamini kuwa Israel "ilijihusisha, inajihusisha na kuna hatari iendelea kushiriki katika vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina huko Gaza." Maoni ambayo Israeli iliita "kashfa ya uppuzi iliyojaa damu". Ili kutetea kesi hii ya kwanza iliyoletwa na nchi mbele ya ICJ, Pretoria inatuma "timu ya wasomi" ya wanasheria, amebainisha Cathleen Powell, profesa wa sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Cape Town.

Miongoni mwao, John Dugard, mshirika katika ofisi ya wanasheria ya International Doughty Street Chambers, ambayo Amal Clooney ni mali yake. Wakili Dugard alikuwa ripota maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika maeneo ya Palestina.

Pia ni pamoja na Tembeka Ngcukaitobi, ambaye alishughulikia kesi iliyompeleka rais wa zamani Jacob Zuma gerezani. Ujumbe unaoongozwa na Waziri wa Sheria, Ronald Lamola, pia unakwenda Hague kuunga mkono mpango huo.

"Suala la kanuni"

Ombi la la malalamiko la Pretoria limechochewa na sababu za kihistoria na kisiasa, kulingana na waangalizi. Chama tawala (ANC, African National Congress) kwa muda mrefu kimeunga mkono hoja ya Palestina, ambayo ilihusisha na mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi. Nelson Mandela alithibitisha kwamba uhuru wa Afrika Kusini "usingekuwa kamili bila uhuru wa Wapalestina".

Rais Cyril Ramaphosa alitangaza wiki hii kwamba Mandela alikuwa amechochea hatua mbele ya haki ya kimataifa, na kuibua "swali la kanuni": "Watu wa Palestina wanapigwa mabomu, wanauawa (...) Tulikuwa na wajibu wa kusimama na kuunga mkono Wapalestina.

Motisha za Pretoria pia ni za ndani, kulingana na wachambuzi. Kwa mara ya kwanza katika historia yake, ANC iko katika hatari ya kupoteza wingi wake wa wabunge wakati wa uchaguzi ujao uliopangwa kati ya mwezi Mei na Agosti, katika mazingira magumu ya kijamii na kiuchumi.

ANC inaona katika hatua hii "msingi wa kurejesha ukuu uliopotea katika kipindi cha miaka 30 iliyopita na utawala ukiacha kanuni zake taratibu", anaeleza Sara Gon, wa Taasisi ya Mahusiano ya Rangi. Afrika Kusini inawapa hifadhi jamii kubwa zaidi ya Wayahudi katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Lakini nchi hiyo ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu, ambayo sehemu yake inaweza kuona Israeli kwa jicho baya.

Afrika Kusini pia inaweza kupata nafasi katika eneo la kimataifa kwa mbinu yake, anasema Bi. Gon. Mwanachama wa Brics (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini), Pretoria inachukulia kundi hili kama mzani wa kukabiliana na mpangilio wa dunia unaotawaliwa na Marekani na Ulaya. Na Pretoria iliunga mkono kikamilifu upanuzi wa umoja huo, hasa kwa Iran, mpinzani mkuu wa Israeli.

Israel iliapa "kuiangamiza" Hamas baada ya shambulio lake la kiwango kikubwa katika ardhi ya Israel mnamo Oktoba 7 ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,140, ​​hasa raia, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP kupitia data rasmi ya Israeli.

Tangu wakati huo, mashambulizi ya anga ya Israel yamefanya sehemu kubwa za Ukanda wa Gaza kuwa magofu, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 23,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto wadogo, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas. Takriban wakaazi milioni 2.4 wa Ukanda wa Gaza, ambapo karibu milioni 1.9 ambao wamelazimika kukimbia makazi yao kulingana na Umoja wa Mataifa, wanaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.

Maamuzi ya ICJ ni ya mwisho na yana nguvu kisheria, lakini haina uwezo wa kuyatekeleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.