Pata taarifa kuu

Amerika Kusini na Afrika zakabiliwa na rekodi ya wimbi la Joto

Idadi hiyo imeenea ulimwenguni kote: 62.3°C ilihisiwa wikendi iliyopita huko Rio de Janeiro, rekodi ya wimbi la joto. Hata hivyo, hizi zinakusanyika karibu kila mahali kwenye sayari, kutoka Morocco hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na Thailand, Costa Rica na hata Afrika Kusini.

Muonekano wa angani wa ufuo wa Rio de Janeiro wakati wa wimbi la joto mnamo Machi 17, 2024, wakati nchi inakabiliwa na wimbi la joto ambalo halijawahi kushuhudiwa. Wikendi iliyopita, halijoto ilifikia 62.3°C ilihisiwa huko Rio de Janeiro.
Muonekano wa angani wa ufuo wa Rio de Janeiro wakati wa wimbi la joto mnamo Machi 17, 2024, wakati nchi inakabiliwa na wimbi la joto ambalo halijawahi kushuhudiwa. Wikendi iliyopita, halijoto ilifikia 62.3°C ilihisiwa huko Rio de Janeiro. © TERCIO TEIXEIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Digrii 38 nchini Morocco, 42.3 nchini Afrika Kusini, 35.9 huko Franceville nchini Gabon, 45 nchini Sudan Kusini… Kwa upande mwingine wa Atlantiki, 39.7 nchini Colombia, 37.4 Guyana, 39 .2 nchini Costa Rica. Tukivuka Bahari ya Pasifiki, 36.2 nchini Indonesia, au hata 36.3 nchini Vietnam. Litania inaweza kuendelea zaidi, marudio ya kusikitisha ya rekodi za joto zilizovunjwa katika siku za hivi karibuni kote ulimwenguni, ziwe za kila mwezi au hata rekodi kamili.

"Ni ongezeko la joto duniani kwa asili ya binadamu, ambalo linapiga, hasa katika ulimwengu wa kusini na karibu na ikweta," anaeleza Davide Faranda, mtafiti wa CNRS katika maabara ya sayansi ya hali ya hewa na mazingira. "Afrika yote imeathiriwa na halijoto zaidi ya tulivyoona hivi majuzi. "

Juba, Sudan Kusini, yakabiliwa na wimbi la joto

Hii inathibitishwa na digrii 45 zilizotangazwa nchini Sudan Kusini, ambazo zilisababisha mamlaka kufunga shule hadi ilani nyingine, kwa sababu wengi wao hawajaunganishwa na umeme na hawawezi kutumia feni. Ikiwa wimbi la joto linaloikumba Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, litahisiwa vikali na kila mtu, Waislamu wanateseka zaidi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Sadik Umar Mohammed, mfanyabiashara wa Sudan katika soko la Souk Libya, amemaliza sala yake hivi punde: “Kwa kweli kuna joto kali, tunajitahidi kukabiliana nalo. Wimbi hili la joto linachosha kila mtu hapa. Kwa sababu hata usiku joto halipungui,” anaambia mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux.

Chini ya jua kali la adhuhuri, kila kitu hakituliia sokoni, kama vile Keflé, mfanyabiashara mwingine kutoka Eritrea, anasema hivi: “Joto hili haliwezi kuvumilika kabisa! Wateja wetu wanakaa nyumbani. Wanakuja tu baada ya saa kumi Alaasiri.… Kwa siku nzima, hatuuzi chochote. "

Akiwa ameketi chini ya mwavuli, milundo midogo ya embe iliyopangwa kwenye mkeka, Khamisa Suleiman anashikilia chupa kubwa ya maji. Bila shaka angependelea kutokuwepo hapa, lakini hana chaguo. “Hali hii ni ngumu. Watoto wangu hawana chakula cha kutosha, sina cha kuwalipia karo zao za shule. Kwa hivyo ni lazima nije kufanya kazi hapa chini ya jua,” anaeleza. Mamlaka imependekeza kwamba wazazi wasiwaruhusu watoto wao kucheza nje. Joto linatarajiwa kuendelea kwa angalau siku kumi.

Afrika inakabiliwa na ukosefu wa hewa

Lakini hali hiyo haiko Sudan Kusini pekee, "wimbi la joto liko barani Afrika kwa sasa," anaelezea Davide Faranda. Rekodi zinavunjwa katika sehemu kubwa ya bara la Afrika. "

Ramani ya Afrika Kaskazini inayoonyesha hitilafu za halijoto ikilinganishwa na wastani, Machi 18, 2024 saa 2 usiku za Afrika ya Kati.
Ramani ya Afrika Kaskazini inayoonyesha hitilafu za halijoto ikilinganishwa na wastani, Machi 18, 2024 saa 2 usiku za Afrika ya Kati. © European Centre for Medium-range Weather Forecasts (ECMWF)
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.