Pata taarifa kuu

Joe Biden: Mabadiliko ya hali ya hewa ni 'tishio lililopo'

Rais wa Marekani amechukua msururu wa hatua kuelewa vyema viwango vya juu vya joto huku nchi yake ikiathiriwa na mawimbi ya joto kali.

Joe Biden ametangaza mfululizo wa hatua, unaofadhiliwa na mpango mkubwa wa uwekezaji wa mpito wa nishati.
Joe Biden ametangaza mfululizo wa hatua, unaofadhiliwa na mpango mkubwa wa uwekezaji wa mpito wa nishati. AFP - ALESSANDRO RAMPAZZO
Matangazo ya kibiashara

"Sidhani kama bado inawezekana kwa mtu yeyote kukataa athari za mabadiliko ya hali ya hewa," Joe Biden amesema. Siku ya Alhamisi Julai 27, rais wa Marekani alitangaza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni "tishio lililopo" wakati "zaidi ya Wamarekani milioni 100" wanakabiliwa na joto kali.

Rais huyu kutoka chama cha Democratic mwenye umri wa miaka 80 alisema joto linasababisha vifo vingi kuhusina na hali ya hewa na na mabadiliko ya tabia nchi nchini Marekani, na kusababisha vifo vya watu 600 kwa mwaka, zaidi ya mafuriko na vimbunga. Hasa, alichukua mfano wa mwanamke ambaye aliungua vibaya sana baada ya kuanguka kutoka kwa kiti chake cha magurudumu kwenye eneo lenye joto kali huko Arizona, kusini-magharibi mwa Marekani.

Mfululizo wa hatua za kukabiliana na joto

Wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebaini hivi punde kwamba dunia sasa iko katika "zama za kuchemka" na haiko tena katika "zama za joto", Joe Biden ametangaza mfululizo wa hatua, unaofadhiliwa na mpango mkubwa wa uwekezaji wa mpito wa nishati. Tayari zimeidhinishwa na Baraza la Congress, na zinalenga kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji katika magharibi mwa Marekani na kuboresha mfumo wa kitaifa wa utabiri wa hali ya hewa.

Pia aliahidi ulinzi zaidi kwa wafanyakazi walio wanaokabiliwa zaidi kwa viwango vya joto, hasa katika kilimo na ujenzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.