Pata taarifa kuu

Joe Biden atafuta marafiki Kusini mwa Amerika

Marekani ni mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Amerika huko Los Angeles wiki hii. Joe Biden anataka kuchukua fursa ya mkutano huu kuzindua upya ushirikiano na kuimarisha uchumi kati ya nchi za kaskazini na kusini mwa bara hilo.

Katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Amerika, unaoanza Jumatatu hii, Juni 6, Rais wa Marekani Joe Biden atakuwa na mengi ya kufanya ili kuzishawishi nchi za Amerika Kusini kupendelea Marekani kuliko China.
Katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Amerika, unaoanza Jumatatu hii, Juni 6, Rais wa Marekani Joe Biden atakuwa na mengi ya kufanya ili kuzishawishi nchi za Amerika Kusini kupendelea Marekani kuliko China. AP - Carolyn Kaster
Matangazo ya kibiashara

Mkutano mkuu, unaotakwa na rais wa Marekani, unaweza kugeuka kuwa mgongano wa kisiasa. Bado hakujakuwa na matuimaini ya kushiriki kwa nchi nyingi katika mkutano huu.

Kufanyika kwa mkutano huu kumegeuka kuwa jinamizi la kidiplomasia kwa utawala wa Biden, ameripotoi mwandishi wetu huko New York, Loubna Anaki.

Je, Mexico itasusia mkutano huo?

Asili: Uamuzi wa Ikulu ya White House kuzitenga Cuba, Venezuela na Nicaragua kwenye orodha ya wageni, ikisema kwamba "nchi hizi za kiimla hazikaribishwi kwa sababu ya ukiukaji wao wa haki za binadamu" .

Kwa kujibu, nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Mexico, zimetishia kususia mkutano wa Los Angeles. Kushiriki kwa Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador (anayejulikana kama AMLO) bado hakujathibitishwa. Mkuu wa nchi wa Mexico amesema atajizuia kushiriki mkutano huo wa tisa ikiwa nchi zote za Amerika hazitaalikwa. Shinikizo la Mexico linaiweka diplomasia ya Biden katika matatizo zaidi.

Mwishoni mwa juma lililopita, Wizara ya Mambo ya Nje ilirejea tena tishio la rais wa Mexico la kususia mkutanohuo kwa kusema kwamba jukumu liko kwenye mahakama ya Marekani, ameripoti mwandishi wa RFI huko Mexico, Gwendolina Duval.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.