Pata taarifa kuu

Uchafuzi wa plastiki: Mazungumzo ya kimataifa yaanza nchini Kenya

Mazungumzo ya kimataifa yameanza siku ya Jumatatu nchini Kenya kujadili hatua madhubuti dhidi ya kuenea kwa taka ambazo "zinaharibu mazingira", kutoka chini ya bahari hadi vilele vya milima.

"Mifumo yote ya ikolojia (...) inatishiwa na uchafuzi wa plastiki," limesema Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment).
"Mifumo yote ya ikolojia (...) inatishiwa na uchafuzi wa plastiki," limesema Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment). © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe kutoka nchi 175 walikubaliana mwaka jana kukamilisha mkataba wa kwanza wa kimataifa wa kukabiliana na janga la plastiki ifikapo mwisho wa mwaka 2024. Iwapo kuna makubaliano mapana juu ya hitaji la mkataba, misimamo inatofautiana kati ya nchi tofauti, watetezi wa mazingira na watengenezaji wa plastiki.

"Uchafuzi wa plastiki unaendelea kufurika bahari zetu, kudhuru wanyamapori na kuingia kwenye mifumo yetu ya ikolojia. Hii inaleta tishio la moja kwa moja kwa mazingira yetu, afya ya binadamu na usawa dhaifu wa sayari yetu," amesema mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment), Gustavo Meza-Cuadra Velasquez, katika ufunguzi wa mazungumzo hayo, yatakayomalizika Jumapili jijini Nairobi.

Madau katika mazungumzo haya ni ya juu kwa sababu plastiki, inayotokana na kemikali za petroli, iko kila mahali: upotevu wa ukubwa wote tayari unapatikana chini ya bahari na juu ya milima. Microplastics imegunduliwa katika damu au maziwa ya mama.

"Mifumo yote ya ikolojia (...) inatishiwa na uchafuzi wa plastiki", amebaini Jyoti Mathur-Filipp, katibu mtendaji wa INC kabla ya kudai kwamba "tunashikilia uwezo mikononi mwetu kusahihisha mwelekeo huu.

"Kulinda binadamu"

Wapatanishi tayari wamekutana mara mbili, lakini mkutano wa Nairobi, makao makuu ya Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP), unatoa fursa ya kwanza kujadili rasimu ya mkataba iliyochapishwa mwezi Septemba ambayo inaelezea njia nyingi za kutatua tatizo hilo. Kabla ya mijadala ya Nairobi, karibu nchi sitini zilitoa wito wa "vifungu vya kisheria katika mkataba ili kuzuia na kupunguza matumizi na uzalishaji" wa plastiki.

Mashirika mengi yasiyo ya kiserikali pia yamesihi siku ya Jumatatu kwa mkataba kabambe. Kulingana na Marian Ledesma, wa Greenpeace, ili "kuepusha matokeo yasiyoweza kurekebishwa ya shida ya hali ya hewa", uzalishaji wa plastiki ulipaswa kupunguzwa kwa 75% ifikapo 2040. Lakini msimamo huu haungwi mkono na nchi wanachama wa OPEC, Marekani na washawishi wa tasnia ya plastiki ambao wanasitasita kuzingatia kupunguzwa kwa uzalishaji na wanafanya kampeni kupendelea kuchakata tena.

"Mkataba kuhusu plastiki unapaswa kuzingatia kukomesha uchafuzi wa plastiki, sio uzalishaji wa plastiki," International Council of Chemical Associations, ambalo linatetea nafasi za wazalishaji wa plastiki, limeliambia shirika la habari la AFP.

Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea kimazingira pia yamekejeli kuundwa kwa muungano, ikiwa ni pamoja na Iran, Saudi Arabia na Urusi - wazalishaji wakuu wa mafuta - ambao WWF inasema inatetea kupendelea "mbinu ya hiari na iliyodhamiriwa kitaifa, badala ya kufunga sheria za kimataifa".

Kuzidisha hali mbaya

Kuundwa kwa muungano huu "si jambo la kushangaza," amesema Carroll Muffett, mkurugenzi wa Kituo cha sheria ya kimataifa ya mazingira (CIEL), lakini "hiyo haitoi udhuru kwa nchi zingine kuonyesha nia."

Uchafuzi wa plastiki unatarajiwa kuwa mbaya zaidi: uzalishaji wa kila mwaka umeongezeka zaidi ya mara mbili katika miaka 20 hadi kufikia tani milioni 460. Inaweza kuongezeka mara tatu ifikapo 2060 ikiwa hakuna kitakachofanyika. 

Plastiki pia ina jukumu katika ongezeko la joto duniani: iliwakilisha 3.4% ya uzalishaji wa hewa duniani mwaka 2019, takwimu ambayo inaweza kuwa zaidi ya mara mbili ifikapo 2060, kulingana na OECD. Mazungumzo ya Nairobi yanakuja wiki chache kabla ya kuanza kwa COP 28 kuhusu tabia nchi katika Umoja wa Falme za Kiarabu, lengo ambalo ni kufikia upunguzaji wa utoaji wa gesi chafuzi.

Mkutano huo wa Nairobi ni wa tatu kati ya vikao vitano katika mchakato wa kuharakishwa unaolenga kuhitimisha mazungumzo hayo mwaka ujao. Baada ya mji mkuu wa Kenya, mazungumzo yataendelea mwezi wa Aprili 2024 nchini Canada na kuhitimishwa nchini Korea Kusini mwishoni mwa mwaka 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.