Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Wafungwa wa FARDC na watoto wafariki dunia katika kambi ya jeshi

Vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa sasa vinendesha mashambulizi dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo. Lakini, wapiganaji wanaokamatwa huwa wakiambatana na wake zao na watoto na kwa sasa wamefungwa katika mazingira mabaya ya kibinadamu.

Askari wa FARDC
Askari wa FARDC © KUDRA MALIRO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa Rais Félix Tshisekedi alipongeza jeshi lanchi hiyo, FARDC, kwa kuharibu zaidi ya 95% ya ngome za kundi la waasi la CNRD katika Eneo la Kalehe mkoani Kivu Kusini na kukamata watu 1,700, ikiwa ni pamoja na wapiganaji 245.

Karibu watu 2000 wamefungwa katika kambi ya kijeshi ya Nyamuyinyi. Watu watano wakiwemo watoto walifariki dunia siku ya Ijumaa kutokana na hali duni ya maisha inayowakabili wafungwa hao katika kambi hiyo. Tangu mwanzoni mwa mwezi Desemba, watu kadhaa wamefariki dunia kutokana na utapiamlo mkubwa au mdongamano kwa sababu wafungwa wamezuiliwa katika sehemu ndogo na ni vigumu kupata hewa, chanzo cha Umoja wa Mataifa kimebaini.

Ripoti ambayo, imepelekea shirika la Umoja wa Mataifa linalojihuisha na masuala ya binadamu OCHA kuamua kuvunja ukimya. Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu "ilielezea wasiwasi wake mkubwa" kuhusu hali ya watu 2000 wanaozuiliwa katika kambi ya kijeshi ya Nyamuyinyi : "mamia kati yao ni wagonjwa, haswa wazee na watoto" , limeonya shirika hilo la Umoja wa mataifa, ambalo limeshtumu 'hali za usafi mdogo na za usalama, uhaba wa maji safu, huduma mbovu ya afya na chakula'.

Ripoti hii ilitolewa baada ya ujumbe wa OCHA kuweza kuingia kambini Jumatano na Alhamisi ukiambatana wajumbe wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO. Ziara hii, iliyokubaliwa na viongozi wa DRC baada ya mazungumzo ya siku kadhaa, hakuweza kupelekea wajumbe hao kutathmini idadi ya raia wanaozuiliwa katika kambi hiyo, ingawa ni wengi, kwa mujibu wa mashahidi.

Kutokana na hali hiyo, David Mac Lachlan-Karr, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, amekumbusha viongozi wa DRC kwamba 'wana jukumu la kuheshimu utu na kanuni za kibinadamu'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.