Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Maambukizi ya Ebola yaendelea kuripotiwa Mashariki mwa DRC

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema zimerekodi visa vipya 23 vya wagonjwa wa Ebola katika kipindi cha siku nne mashariki mwa nchi hiyo ambako kunashuhudiwa machafuko.

Wafanyakazi wa afya wanajiandaa kutoa chanjo dhidi ya Ebola katikati mwa mji wa Goma, mashariki mwa DRC.
Wafanyakazi wa afya wanajiandaa kutoa chanjo dhidi ya Ebola katikati mwa mji wa Goma, mashariki mwa DRC. REUTERS/Djaffer Sabiti
Matangazo ya kibiashara

Serikali inasema visa 10 peke yake viliripotiwa kwenye mji wa Mabalako jimboni Kivu Kaskazini, ambapo sita kati yao ni waganga wa kienyeji.

Jumatano ya wiki hii watu watatu waliripotiwa kuwa na maambukizi jimboni Kivu Kaskazini, eneo ambalo halikuwa limeripotiwa mgonjwa mpya kwa siku zaidi ya 85.

Hivi karibuni Shirika la kimataifa la Madaktari swasiokuwa  na Mipaka MSF lilitangaza kusitisha shughuli zake kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika  mkoa wa Ituri kutokana na kile ilichosema ni mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi dhidi ya wafanyakazi wake walioko mstari wa mbele kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Ive Ndjadi afisa wa juu wa MSF, alisema vitisho dhidi ya wafanyakazi hao wa afya lakini pia miundo mbinu muhimu ya kusaidia katika mapambano hayo, imeharibiwa.

Mashirika ya kiraia yanahofia kuwa, kuondoka kwa maafisa wa MSF kunaweza kusababisha maambukizi zaidi, wakati huu Professa Jean-Jacques Muyembe anayeongoza kamati ya kupambana na maambukizi ya Ebola, akitoa wito kwa wakaazi wa eneo hilo kuendelea kushirikiana kutokomeza ugonjwa huo.

Wataalamu wameonya kuhusu kuongezeka kwa visa vya wagonjwa, ambapo mpaka sasa watu zaidi ya 1800 wameshapoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.