Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

DRC: Timu zinazopambana dhidi ya Ebola zalengwa katika mashambulizi Ituri

Maafisa wanaopambana dhidi ya Ebola Mashariki mwa DRC wamelengwa katika mashambulizi mapya usiku wa Jumatatu kuamkia Alhamisi wiki hii.

Afisa wa afya wa DRC anayepambana dhidi ya Ebola katika hospitali ya Bwera, karibu na mpaka na Uganda (picha ya kumbukumbu).
Afisa wa afya wa DRC anayepambana dhidi ya Ebola katika hospitali ya Bwera, karibu na mpaka na Uganda (picha ya kumbukumbu). © REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Ukosefu wa usalama unatatiza zoezi la mapambano dhidi ya ugonjwa huo, haswa katika mkoa wa Ituri.

Shambulio la kwanza lililenga kambi ya Shirika la Afya Duniani (WHO), iliyoko Biakato, Jumatano usiku kati ya usiku wa manane na saa nane usiku.

Kulingana na ripoti ya kwanza iliyotumwa na vyanzo vya Umoja wa Mataifa, watu watatu wamepoteza maisha wakati wa shambulio hilo.

Mfanyakazi wa Wizara ya Afya ya DRC, pamoja na madereva wawili waliotumwa na shirika la Afya Duniani (WHO) ni miongoni mwa waliouawa. Watu watano wamejeruhiwa na mmoja ametoweka. Magari kadhaa pia yalichomwa moto kwenye eneo hilo.

Kwingineko ambapo shambulio lilitokea ni katika kituo kinachoshughulikia wagonjwa wa Ebola cha Mangina, katika wilya ya Beni, kilomita zaidi ya hamsini na Ituri. Mshambuliaji mmoja aliuawa katika shambulio hilo baada ya vikosi vya usalama kuingilia kati.

Kwa sasa viongozi wanachunguza kama mashambulizi haya mawili yalitekelezwa na kundi moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.