Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi DRC waahirishwa hadi Desemba 30

Tume ya Uchaguzi nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo (CENI) imetangaza kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa umepangiwa kufanyika Jumapili Desemba 23 hadi Jumapili Desemba 30, 2018.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI) Corneille Nangaa katika mkutano na waandishi wa habari Kinshasa.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC (CENI) Corneille Nangaa katika mkutano na waandishi wa habari Kinshasa. Photo: Luis Tato/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume Corneille Nangaa amesema, uamzi huo umefikiwa baada ya ghala la CENI kuteketea kwa moto wiki iliyopita. CENI inasema baada ya kuandaa kikao na waakilishi wa vyama vya kisiasa waliamua kuchukuwa uamzi wa kuahirisha uchaguzi hadi Desemba 30.

Mwenyekiti wa Ceni amesema kabla ya kuchukuwa uamuzi huo, walikubaliana na wanasiasa mbalimbali kuahirisha uchaguzi kwa wiki moja ili waweze kupata vifaa vya uchaguzi kwa mkoa wa Kinshasa.

Corneille Nangaa amesema uchaguzi hauwezi kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini DRC bila kuemo mkoa wa Kinshasa ambao ulipoteza vifaa vya uchaguzi, baada ya ghala moja kuu lililokuwa likihifadhi vifaa hivyo kuteketea kwa moto.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamekosoa hatua hiyo, huku upinzani ukitarajia kutoa msimamo wake rasmi baadaye.

Chanzo kutoka CENI ambacho hakikutaja jina lake kimesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuchelewa kwa shughuli ya kufikisha vifaa na mitambo ya kupigia kura vituoni.

Mapema wiki iliyopita Mwenyekiti wa CENI alitangaza kwamba vifaa vyote vimewasili katika maeneo mbalimbali nchini na maandalizi yamekamilika.

Uchaguzi wa DRC umekuwa ukisogezwa mbele kwa zaidi ya miaka miwili sasa, huku rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila akishutumiwa kwa kutoa visingizio kadhaa vya kuahirisha uchaguzi ili aendelee kusalia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.