Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-SIASA

Makabiliano yazuka baada ya kusitishwa kwa kampeni ya uchaguzi Kinshasa

Mapigano kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya polisi yamezuka katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, ambapo gavana wa mkoa huo aliamuru kusitishwa kwa kampeni ya uchaguzi wa urais katika mji wa Kinshasa.

Vikosi vya usalama katika mji wa Kinshasa, DRC.
Vikosi vya usalama katika mji wa Kinshasa, DRC. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Gavana Andre Kimbuta alichukuwa uamuzi huo Jumatano wiki hii baada ya kuzuka machafuko ambapo watu saba walipoteza maisha na masanduku 1,000 ya kura yaliteketezwa kwa moto wiki iliyopita.

Makabiliano katika mji wa Kinshasa yalizuka saa chache baada ya kutangazwa kusitishwa kwa kampeni ya uchaguzi katika mji mkuu wa nchi hiyo kubwa Afrika ya kati. Hatua hiyo iliwakasirisha wafuasi wa mmoja wa wagombea wa upinzani Martin Fayulu.

Vikosi vya usalamam vilitumia mabomu ya machozi ili kuzuia wafuasi wa Fayulu kwenda kwenye sehemu ambapo kumekuwa kumeandalia mkutano wa uchaguzi katika moja ya vitongoji vya mji wa Kinshasa.

Tume ya Uchaguzi ilikanusha Jumatano jioni taarifa iliyorushwa na vyombo kadhaa vya habari nchini humo kwamba uchaguzi uliopangwa kufanyika Jumapili Desemba 23 umeahirishwa.

Uchaguzi unaokabiliwa na mvutano wa kisiasa, unatarajia kumteua mrithi wa Joseph Kabila, madarakani tangu mwaka 2001.

Gavana Kimbuta ameongeza kuwa wagombea wanaweza tu kuendesha kampeni zao katika vyombo vya habari.

Hata hivyo wadadisi wanasem aKinshasa ni ngome kubwa ya upinzani, kwa hiyo utawala uogopa kupoteza kura katika mkoa huo, na hivyo kutumia mbinu ya kusitisha kampeni za uchaguzi katika mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.