Pata taarifa kuu
DRC-USALAM-SIASA

Watu 45 wauawa katika machafuko Magharibi mwa DRC

Watu 45 wameuawa katika mapigano ya kikabila kuanzia Jumapili iliyopita Magharibi mwa DRC na kusababisha watu kukimbilia nchi jirani ya Congo Brazaville, siku chache kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Jumapili.

Ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini DRC siku nne kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 23, 2018.
Ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini DRC siku nne kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 23, 2018. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa Jimbo la Mai-Ndombe Gentiny Ngobila amesema mauaji hayo yalitokea kuanzia usiku wa Desemba 15 kuamkia Desemba 16 ambapo takwimu za awali zinaonyesha kuwa watu 45 wameuawa wengine 60 wamejeruhiwa.

Mkoa wa Mai-Ndombe uliopo karibu na mto Congo unaogawana kati ya DRCongo na Congo Brazaville unakaliwa na watu wengi wenye kujihusisha na kilimo pamoja na Uvuvi. Usalama umerejea baada ya kutumwa kwa vikosi vya jeshi na polisi kutuliza ghasia.

Kiongozi wa eneo hilo amesema machafuko hayo hayana uhusiano wowote na kampeni za uchaguzi, siku 5 kabla ya kupiga kura.

Hayo yanajiri wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetolea wito pande zote husika na uchaguzi huo kujiepusha na hali yoyote ile inayoweza kusababisha vurugu hususan katika kutoa matamko na kuitaka serikali ya Kinshasa kuhakikisha usalama wa wagombea unadhaminiwa.

Licha ya kupongeza hatua chanya za kiufundi kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi, baraza hilo limesema linatiwa wasiwasi na matukio hasi yalioshuhudiwa katika siku za nyuma yaliosababisha mauaji na uharibifu mkubwa wa vitu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.