Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-UCHAGUZI

Felix Tshisekedi atatimiza ndoto ya baba yake?

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanapiga kura siku ya Jumapili.

Félix Tshisekedi, mgombea wa urais nchini DRC
Félix Tshisekedi, mgombea wa urais nchini DRC JUNIOR D. KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatimaye, taifa hilo la Afrika ya Kati, lenye zaidi ya watu Milioni 80, litakuwa na rais mpya, baada ya miaka 17.

Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila Kabange, hawanii nafasi hiyo kwa sababu amezuiwa kikatiba.

Katiba ya DRC, inaeleza kuwa rais anastahili kuongoza nchi hiyo kwa mihula miwili, kila muhula wa miaka mitano.

Mmoja wagombea urais, ni Felix Tshisekedi Tshilombo, mwenye umri wa miaka 55 anayetarajiwa kutoa ushindani mkali katika uchaguzi huo wa kihistoria.

Ni mtoto wa kiume wa mwanasiasa mkongwe wa kisiasa Etienne Tshisekedi aliyefariki dunia Februari mwaka 2017 akiwa nchini Ubelgiji, akiendelea kuwa na ndoto ya kuwa rais.

Tangu miaka ya 80, Tshisekedi alikuwa anawania urais hadi mwaka 2016, na kudai kuibiwa.

Vital Kamerhe (Kushoto) na  Félix Tshisekedi (Kulia) baada ya kukubaliana kuunganisha nguvu kuelekea Uchaguzi Mku wa urais Novemba 28 2018
Vital Kamerhe (Kushoto) na Félix Tshisekedi (Kulia) baada ya kukubaliana kuunganisha nguvu kuelekea Uchaguzi Mku wa urais Novemba 28 2018 AFP/Yasuyoshi Chiba

 

Swali kubwa linaloulizwa na raia wengi wa DRC, ni je, Felix Tshisekedi atatimiza ndoto ya baba yake ?

Kabla ya kuwania urais, Felix, alikuwa amekubaliana na wanasiasa wengine wa upinzani kumuunga mkono Martin Fayulu, ambaye anawakilisha muungano wa Lamuka.

Hata hivyo, aliamua kuwania akiungwa mkono na Vital Kamerhe kutoka chama cha UNC.

Iwapo atashinda Uchaguzi wa Jumapili, Tshisekedi anasema kazi kubwa ni kupambana na ufisadi, janga ambalo anasema limekuwa la taifa.

Aidha, anaahidi kuwa atapandisha kipato cha kila raia wa nchi hiyo kutoka Dola 1.25 kwa siku hadi Dola 11.75.

Tshisekedi anaamini kuwa, kufanikiwa katika hilo, anahitaji muda wa miaka 10 kutekeleza ahadi zake anazosema zitagharimu Dola Bilioni 86.

“Ni kweli, sina uzoefu katika uongozi mbaya, katika kuliendeleza taufa letu, “ Lakini nina uzoefu wa kuheshimu haki za binadamu na maslahi ya kiraia,” amewahi kusema Tshisekedi katika mkutano na Wanahabari.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa kwa sababu ya mgawanyiko wa upinzani, haitakuwa rahisi kwa Tshisekedi kushinda urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.