Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Mauaji Kinshasa: Ofisi ya mashitaka na polisi waanzisha uchunguzi

Polisi na ofisi ya mashitaka wameanzisha uchunguzi baada ya miili minne ya watu waliouawa kugunduliwa katika mji wa Kinshasa. Watu hao waliuawa katika mazingira ya kutatanisha, polisi ya DRC imetangaza Alhamisi wiki hii.

Gari ya polisi ikipiga doria katika mitaa ya Kinshasa.
Gari ya polisi ikipiga doria katika mitaa ya Kinshasa. Junior D. KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumapili alfajiri, miili mitatu ilipatikana katika uwanja wa mpira wa kikapu katika wilaya ya mji wa Kalamu , ikiwa ni pamoja na mwili wa mchezaji wa mira wa kikapu. Mwili wa nne uligunduliwa katika eneo jirani la Yolo, kulingana na ushuhuda kadhaa uliokusanywa na AFP kutoka kwa wakaazi wa eneo hilo.

Mashahidi wengine waliiambia AFP kwamba waliona miili sita kwenye Mto Kalamu, karibu na Matonge, eneo jingine la mkoa huo.

"Polisi wameanzisha uchunguzi. Na Ofisi ya mashitaka pia inaendesha uchunguzi ili kutoa mwanga kuhusu kesi hii," Mkuu wa polisi mjini Kinshasa Jenerali Sylvano ameliambia shirika la Habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.