Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Wafuasi wa upinzani wakamatwa kabla ya kuwasili kwa Tshisekedi Lubumbashi

Wafuasi kadhaa wa upinzani walikamatwa siku ya Jumapili (Oktoba 23) mjini Lubumbashi walipokuwa wakihudhuria mkutano wa maandalizi kwa kuwasili kwa Felix Tshisekedi Jumatatu hii katika katika mji huo.

Wafuasi wa upinzani wamekamatwa siku moja kabla ya kuwasili kwa Felix Tshisekedi mjini Lubumbashi.
Wafuasi wa upinzani wamekamatwa siku moja kabla ya kuwasili kwa Felix Tshisekedi mjini Lubumbashi. REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa viongozi wa mkoa, watu waliokamatwa walikuwa barabarani, wakati ambapo upinzani unadai kuwa polisi walikwenda kuwatafuta kwenye makao makuu ya chama cha UDPS.

Wakati wa tukio hilo, kamishna wa polisi wa mkoa huo, Jenerali Paulin Kyungu mwenyewe, alikuwa akiongoza operesheni kwenye makao makuu ya UDPS. Habari hii imethibitishwa na mkuu wa mkoa wa Haut-Katanga, Pande Kapopo, akihojiwa kwenye simu. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa mkoa, watu waliokamatwa walikuwa mitaani, wakati ambapo sheria iliyowekwa miezi kadhaa iliyopita inasema maandamano yanaruhusiwa kwa idhini ya kiongozi wa manispaa ya jiji.

Upinzani kwa upande wao, wanashtumu polisi kuwakamata wafuasi hao ndani ya makao makuu ya chama cha UDPS na kuwa vifaa vya sauti vilikamatwa. Viongozi tawala katika mkoa huo na upinzani bado hawajakubaliana kuhusu ziara ya Félix-Antoine-Tshisekedi mjini Lubumbashi.

"Atawasili na atapokelewa kwenye uwanja wa ndege, kisha polisi itachukua jukumu la usalama wake," amesema gavana wa mkoa wa Haut-Katanga na kuongeza kuwa wafuasi wa upinzani wanatakiwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na viongozi wa mkoa . Lakini upinzani unadai kuwa, baada ya kuwasili kwa Tshisekedi, kutakua na msafara wa kuzunguka mji wa Lubumbashi mapema asubuhi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wafuasi wengi wa upinzani ambao walikua wakielekea Jumatatu hii, Oktoba 23 katika uwanja wa ndege wa Lubumbashi kumpokea kiongozi wao walitawanyika na polisi wakitumia gesi ya machozi. Wawili wao walikamatwa na polisi wa kuzima ghasia waliotumwa mapema asubuhi katika mji huo.

Umoja wa Mataifa umetoa wito Jumatatu hii Oktoba 23 kwa serikali ya DRC kuachilia huru mara moja wafuasi wa upinzani waliokamatwa jsiku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.