Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA-SIASA

DRC kuwania nafasi kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unatazamia kupiga kura Jumatatu hii Oktoba 16 kuteuwa nchi ambazo zinaweza kujiunga na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu lenye makao yake makuu mjini Geneva, nchini Uswisi.

Ikiungwa mkono na kundi la nchi kumi na tatu za Kiafrika za Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu, DRC inatarajiwa kujiunga na taasisi hiyo. Kura itafanyika Jumatatu hii, Oktoba 16, 2017.
Ikiungwa mkono na kundi la nchi kumi na tatu za Kiafrika za Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu, DRC inatarajiwa kujiunga na taasisi hiyo. Kura itafanyika Jumatatu hii, Oktoba 16, 2017. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ni miongoni mwa nchi zinazowania nafasi hiyo, ambapo Waziri wake wa Haki za Binadamu, Marie-Ange Mushobekwa, yuko New York kwa zaidi ya wiki moja sasa kwa kutetea nchi yake iweze kupata nafasi hiyo. Siku chache zilizopita, mashitrika kimataifa ya kimataifa hamsini ikiwa ni pamoja na yale kutoka DRC yalikua yalipinga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwania kwenye nafasi hiyo yakishtumu "ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu" unaotekelezwa nautawala pamoja na vikosi vyake vya usalama.

"Ni haki kwa mashirika hayo kusema hivyo. Kwa hekima ninayo,ninajiepusha kutaja majina ya nchi ambazo zinataka kujifanya takatifu, wakati tunashuhudia kwa macho yetu maafisa wa polisi wakiwafyatulia risasi raia wasiokua na hatia kutokana na rangi ya ngozi yao au dini yao. Kwa nchi hizo hawasemu lolote. Je, ni kwa sababu nchi hizi zinachukuliwa kuwa na nchi zenye nguvu? ", amesema Marie-Ange Mushobekwa, Waziri wa Haki za Binadamu wa DRC.

Wakati huo huo jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo limesema miili ya watu takriban 26 waliouawa katika shambulio lililofanywa na waasi mapema mwezi huu, imegunduliwa mashariki mwa nchi hiyo.

Watu wote hao walikuwa ni raia wa kawaida isipokuwa mmoja Tu. Mauji hayo yalitokea katika mji wa Eringeti, uliopo kilomita 55 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo wa Beni, mji ambao umekuwa ukikumbwa na misururu ya mashambulio ambayo tayari yamesababisha vifo vya raia 700, kulingana na afisa katika mkoa huo Amisi Kalonda, ambaye amewalaumu waasi kutoka Uganda kwa mashambulio ya hivi karibuni.

Walishambuliwa wakati wakisafiri na gari ndogo ya kukodi.

Jeshi la DR Congo na Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo (Monusco) wamekuwa wakililaumu kundi la wapiganaji wa Uganda la Allied Democratic Forces ADF, kuhusika na mauaji hayo.

Kwa miaka miwili iliyopita eneo linalozingira mji wa Beni limekuwa likikimbwa na mauaji ya kikatili yaliyowauwa mamia ya raia, wengi wao wakichinjwa na kunyongwa hadi kufa.

Maafisa wa DR Congo wamekuwa wakiwalaumu waasi wa ADF kwa mauaji hayo , lakini ripoti kadhaa za wataalam zimekuwa zikisema kuwa makundi mengine, yakiwemo ya wanajeshi wa serikali yalihusika katika baadhi ya mauaji.

Wakati mauaji ya kikatili ya Beni yalipotokea Oktoba 2014, kundi la waasi wa Uganda la ADF walijibu haraka wakishutumu mauaji hayo kutekelezwa na maafisa wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kikosi cha kulinda amani nchini DRC (Monusco).

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, mamlaka za DRC na Umoja wa Mataifa zimeshindwa kuwalinda raia na ADF limesalia kuwa ndilo kundi linalotawala, huku serikali ikisisitiza kuhusu uhusiano wa mauaji hayo na vita vya kidini vya Jihad.

Mauaji haya yanatokea huku mahusiano baina ya jamii ya kimataifa na DRC ukiwa mbaya kutokana na hatua ya rais Josep Kabila kukataa kuachia mamlaka, licha ya muhula wake kumalizika taraehe 20 Disemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.