Pata taarifa kuu
AU

Mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika waanza kutekelezwa

Mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika hatimaye umeanza kufanya kazi Alhamisi ya wiki hii, hatua ambayo umoja wa Afrika unasema una imani kuwa utapanua zaidi soko la bara la Afrika lenye watu bilioni 1.2.

Viongozi wa bara la Afrika wakiwa kwenye picha ya pamoja katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa.
Viongozi wa bara la Afrika wakiwa kwenye picha ya pamoja katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa. Cristiana Soares
Matangazo ya kibiashara

"This is a historic milestone!" tweeted Albert Muchanga, AU commissioner for trade and industry.

Umoja wa Afrika unasema hatua hii italifanya bara la Afrika kufanya biashara za wenyewe kwa wenyewe zitakazofikia thamani ya dola za Marekani trilioni 2.5.

Mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika umeridhiwa na nchi 22 mwezi April mwaka huu, idadi ambayo ndio ilikuwa ikihitajika ili kuufanya uanze kufanya kazi, imesema taarifa ya umoja wa Afrika.

Makubaliano ya kuanza kazi kwa awamu ya kwanza yanatarajiwa kuzinduliwa Julai 7 wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi nchini Niger.

Hatua hii inafikiwa wakati ambapo bado kuna mataifa kadhaa hayajatia saini kuridhia mkataba huu, wakitaka kwanza baadhi ya masuala kupatiwa ufumbuzi, ikiwemo kuboreshwa kwa miundo mbinu, mapambano ya rushwa na kutambua asili ya bidhaa.

Nchi 52 kati ya 55 ambazo ni wanachama wa umoja wa Afrika wametia saini kuazishwa kwa ukanda wa eneo la biashara huria tangu mwezi Machi mwaka 2018 huku Nigeria ambayo inauchumi mkubwa barani Afrika ikiwa ndio nchi pekee haijatia saini.

Hata hivyo nchi nyingine ambazo zinauchumi imara barani Afrika kama vile Kenya, Ethiopia, Misri na Afrika Kusini zenyewe zimetia saini na kuridhia mkataba huu, huku nchi za Zimbabwe na Burkina Faso zikijiunga kuridhia mkataba huu mwezi uliopita.

Umoja wa Afrika unaamini kuwa ukanda wa biashara huria, ikiwa utaridhiwa na nchi zote, utasaidia kuchochea utangamano wa kibiashara baina ya nchi na nchi na kuvutia uwekezaji.

Lengo la umoja wa Afrika kuwa na eneo la biashara huria ni pamoja na kuondolewa kwa vikwazo vya tozo za kibiashara kwenye maeneo ya mipaka, tozo ambazo wataalamu wanasema zinachelewesha utangamano huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.