Pata taarifa kuu
KENYA-SUDAN KUSINI

Ruto: Viongozi msitumie masuala ya kijeshi kisiasa

Naibu wa rais nchini Kenya, William Ruto, amemuonya kinara wa muungano wa upinzani wa Cord, Raila Odinga, kuingilia masuala yanayohusu jeshi la nchi hiyo, matamshi anayoyatoa siku chache tu baada ya kinara huyo kutaka wanajeshi walioko Somalia kurudishwa nyumbani.

Wanajeshi wa Kenya wa KDF, wakiwa wanarejea nyumbani wakitokea Sudan Kusini.
Wanajeshi wa Kenya wa KDF, wakiwa wanarejea nyumbani wakitokea Sudan Kusini. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Naibu wa rais Ruto, amesema kuwa wanasiasa hawapaswi kuingilia masuala ya kijeshi, hasa linapokuja suala la kupelekwa ama kuondolewa kwa wanajeshi wa kulinda amani.

Ruto alikuwa akitetea uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta alioufanya juma moja lililopita, ambapo aliagiza kurejeshwa nyumbani kwa wanajeshi wake walioko Sudan Kusini, saa chache baada ya kufutwa kazi kwa kamanda wa tume ya UNMISS aliyekuwa akitokea Kenya.

Naibu wa rais Ruto, amesema Kenyatta ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, na alikuwa sahihi kuchukua aumuzi wa kuwarudisha nyumbani wanajeshi wetu vile alivyokuwa akiona inafaa.

Ruto amesema uamuz uliochukuliwa na rais ulitokana pia na ushauri alioupata kutoka kwa baraza la usalama la nchi na kwamba suala hili halipaswi kuchukuliwa kisiasa kama ambavyo baadhi wameanza kulichukulia.

Juma lililopita, Raila Odinga, alikosoa namna ambavyo Rais Kenyatta amechukua uamuzi wa kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Kenya kutoka Sudan Kusini, akidai kuwa kutasababisha sintofahamu ya kidiplomasia na jumuiya ya kimataifa.

Odinga alisema uamuzi uliochukuliwa na rais haukuwa uamuzi uliozingatia ushauri mzuri, akisisitiza namna gani jumuiya ya kimataifa imeisaidia nchi yake Kenya hapo kabla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.