Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Maandamano ya kupinga mauaji ya wanawake nchini Kenya

Mamia ya watu wameandamana siku ya Jumamosi mjini Nairobi kupinga mauaji ya wanawake nchini Kenya, wakiwa wamekasirishwa na vifo vya zaidi ya kumi na tano kati yao tangu kuanza kwa mwaka huu.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaitaka serikali kuchukua hatua kuzuia visa hivyo
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaitaka serikali kuchukua hatua kuzuia visa hivyo REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

 

Waandamanaji wameingia katika mitaa ya mji mkuu, wakiwa na mabango yaliyosomeka: "Kuwa mwanamke haipaswi kuwa hukumu ya kifo" na "Ubabe unaua." Wengine walikuwa na majina na picha za wahanga.

Kundi hilo liliimba "Acheni kutuua" walipokuwa wakiandamana kuelekea bungeni, na kusababisha msongamano wa magari kusimama katika eneo kuu la biashara la Nairobi. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, takriban wanawake 16 wameuawa nchini Kenya mwaka huu. Bila kuhusishwa na kila mmoja, mauaji haya yaliangazia unyanyasaji dhidi ya wanawake, "unaongezeka" kulingana na serikali.

Katika mojawapo ya visa vilivyotokea nchini, mwanamke mwenye umri wa miaka 26 aliuawa mnamo Januari 4 katika nyumba fupi ya kukodisha, na mtu anayedaiwa kuwa mwanachama wa genge la wanyang'anyi ambao wanalenga wanawake kupitia maeneo ya makutanio, kulingana na polisi. Takriban wiki mbili baadaye, mwanamke mwenye umri wa miaka 20 alinyongwa, kukatwa vipande vipande na mabaki yake kuwekwa kwenye mfuko wa plastiki. Wanaume wawili walitiwa mbaroni katika kesi hii, lakini bado hawajafunguliwa mashtaka.

"Mauaji ya wanawake ni dhihirisho la kikatili zaidi la unyanyasaji wa kijinsia," limesema shirika la Amnesty International nhini Kenya katika taarifa iliyotolewa kwenye hafla ya maandamano. "Haikubaliki na haipaswi kamwe kuwa ya kawaida," shirika hili la haki limeongeza, likitoa wito kwa mamlaka kuharakisha uchunguzi na mashtaka ya wahalifu.

Katika maandamano hayo, Terry Wangare, afisa wa mawasiliano, amesema ni "wakati wa Kenya kusimama na kufanya uamuzi." "Hakuna anayejali," ameliambia shirika la habari la AFP. Faith Claire Wanjiru, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 ambaye alikuwa akishiriki maandamano yake ya kwanza, amesema "yuko na hasira". "Hakuna mtu anayepaswa kuchukua maisha ya mtu," ameongeza.

Kulingana na waandalizi, maandamano kama hayo yamefanyika katika mikoa 10, ikiwa ni pamoja na katika miji ya Kisumu na Mombasa. Kulingana na ripoti ya serikali iliyotolewa mwaka jana, zaidi ya asilimia 30 ya wanawake nchini Kenya hufanyiwa ukatili wa kimwili maishani mwao na 13% hupitia aina fulani ya ukatili wa kingono. Lakini kulingana na mashirika ya haki za binadamu, hii ni sehemu ndogo tu ya ukweli.

Kulikuwa na takriban mauaji 152 ya wanawake nchini Kenya mwaka jana, kulingana na shirika la Femicide Count, ambalo hufuatilia matukio yaliyoripotiwa pekee. Mwaka 2022, wanawake na wasichana wapatao 725 waliuawa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, kulingana na ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.