Pata taarifa kuu

Mpango wa Nairobi kutuma polisi nchini Haiti ni kinyume na katiba: Mahakama

Nairobi – Nchini Kenya, Mahakama ya juu katika uamuzi wake imesema mpango wa serikali katika taifa hilo la Afrika Mashairiki kuwatuma polisi nchini Haiti kuongoza kikosi cha walinda amani wa UN, ni kinyume na katiba.

Kenya ilisema kuwa iko tayari kupeleka hadi maafisa 1,000 wa polisi nchini Haiti.
Kenya ilisema kuwa iko tayari kupeleka hadi maafisa 1,000 wa polisi nchini Haiti. Β© REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kenya ilikuwa imekubali kuwatuma polisi elfu moja nchini Haiti kusaidia kurejesha usalama pamoja na kupambana na makundi ya watu wenye silaha.

Uamuzi huu wa mahakama unakuja wakati huu ambapo serikali ya Haiti inatoa wito kwa jamii ya kimataifa kutuma kikosi chake kuwasaidia maofisa wake ambao wameonekana kuzidiwa na magenge.

Maofisa wa polisi nchini Haiti wameonekana kulemewa na makundi ya watu wenye silaha wanaowahangaisha raia kwenye taifa hilo
Maofisa wa polisi nchini Haiti wameonekana kulemewa na makundi ya watu wenye silaha wanaowahangaisha raia kwenye taifa hilo Β© Odelyn Joseph / AP

Mwezi Oktoba mwaka jana, baraza la usalama katika Umoja wa Mataifa liliidhinisha mpango huo wa Nairobi licha ya kupingwa na ndani ya nchi.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Kenya, Ekuru Aukot, aliwasilisha kesi katika mahakamani mwaka uliopita kupinga hatua hiyo ya serikali ya rais Ruto.

Haiti imekuwa inakabiliwa na utovu wa usalama unaosababishwa na makundi ya watu wenye silaha
Haiti imekuwa inakabiliwa na utovu wa usalama unaosababishwa na makundi ya watu wenye silaha Β© Odelyn Joseph / AP

Katika uamuzi wake, Jaji Enock Chacha Mwita, ameeleza kuwa hatua yoyote ya serikali au afisa wake kuwatuma polisi nchini Haiti ni kinyume na katiba.

Hadi tukichapisha taarifa hii, serikali ya Nairobi haikuwa imezungumzia uamuzi huo wa mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.