Pata taarifa kuu

Tanzania yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa virusi vya Marburg

Tanzania imetangaza leo Ijumaa kumalizika kwa janga la ugonjwa wa virusi vya Marburg, ugonjwa wa ina moja na Ebola ambao pia husababisha homa ya hemorrhagic, miezi miwili baada ya kuanza kwa maambukizi, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Watu 12 pia walifariki kwa ugonjwa wa virusi vya Marburg huko Equatorial Guinea katika mlipuko wa kwanza ulioripotiwa mnamo Januari 7. Milipuko mingine au kesi za pekee zimeripotiwa huko nyuma huko Afrika Kusini, Angola, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Watu 12 pia walifariki kwa ugonjwa wa virusi vya Marburg huko Equatorial Guinea katika mlipuko wa kwanza ulioripotiwa mnamo Januari 7. Milipuko mingine au kesi za pekee zimeripotiwa huko nyuma huko Afrika Kusini, Angola, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. © CDC/ Dr. Frederick Murphy
Matangazo ya kibiashara

"Jumla ya wagonjwa tisa (wanane walithibitishwa na mmoja anashukiwa kuambukizwa virusi vya Marburg) na vifo sita vilrekodiwa wakati wa mlipuko huo ambao ulitangazwa mnamo Machi 21," WHO imesema katika taarifa. "Mgonjwa wa mwisho iliyethibitishwa hakupatikana na virusi vya Marburg alipofanyiwa vipimo kwa mara ya pili mnamo Aprili 19, hali ambayo ilipelekea kusubiri siku 42 kutangaza kumalizika kwa janga hilo," WHO imebainisha.

Virusi vya Marburg ni pathojeni hatari ambayo husababisha homa kali mara nyingi huambatana na kutokwa na damu kuathiri viungo vingi na kupunguza uwezo wa mwili kufanya kazi vizuri. Ni sehemu ya familia ya filovirus, ambayo virusi vya Ebola pia vinapatikana; Mlipuko wa Ebola umesababisha vifo vingi barani Afrika.

Popo wa matunda wa Kiafrika ndiye mwenye asili ya virusi vya Marburg, ambaye huibeba lakini haugui. Virusi hivyo vilichukua jina lake kutoka katika jiji la Ujerumani la Marburg, ambako vilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1967, katika maabara ambapo wafanyakazi walitangamana na nyani wa kijani walioambukizwa kutoka Uganda. Wanyama wanaweza kusambaza kwa nyani wanaoishi karibu nao, wakiwemo binadamu. Maambukizi ya ndani ya binadamu  hufanyika kwa kugusa damu au maji maji mengine ya mwili.

Kulingana na WHO, kiwango cha vifo vya kesi zilizothibitishwa kilianzia 24% hadi 88% (kwa wastani chini ya 50%) katika magonjwa ya mlipuko ya hapo awali, kulingana na aina ya virusi na matibabu ya wagonjwa. Kwa sasa hakuna chanjo au tiba ya kuzuia virusi hivi, lakini matibabu ya majaribio, ikiwa ni pamoja na vitokanavyo na damu, matibabu ya kinga na matibabu kwa kutumia dawa, yanatathminiwa, WHO imesema.

Watu 12 pia walifariki kwa ugonjwa wa virusi vya Marburg huko Equatorial Guinea katika mlipuko wa kwanza ulioripotiwa mnamo Januari 7. Milipuko mingine au kesi za pekee zimeripotiwa huko nyuma huko Afrika Kusini, Angola, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.