Pata taarifa kuu

Virusi vya Marburg vyaua watu watano nchini Tanzania

Ugonjwa wa ajabu ambao uliwauwa watu watano nchini Tanzania ulitambuliwa kama kutoka kwa virusi vya Marburg, binamu wa Ebola ambao pia husababisha homa ya hemorrhagic, Wizara ya Afya imetangaza Jumanne.

"Majibu ya maabara yetu ya afya ya umma yamethibitisha kuwa ugonjwa huo ulisababishwa na virusi vya Marburg," amesema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, akitoa wito kwa raia kuwa watulivu "kwa sababu serikali imefanikiwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo".
"Majibu ya maabara yetu ya afya ya umma yamethibitisha kuwa ugonjwa huo ulisababishwa na virusi vya Marburg," amesema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, akitoa wito kwa raia kuwa watulivu "kwa sababu serikali imefanikiwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo". © RFI/Igor Strauss
Matangazo ya kibiashara

"Majibu ya maabara yetu ya afya ya umma yamethibitisha kuwa ugonjwa huo ulisababishwa na virusi vya Marburg," amesema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, akitoa wito kwa raia kuwa watulivu "kwa sababu serikali imefanikiwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo".

Wagonjwa watatu wamelazwa hospitalini na watu 161 waliotangamana nao wanafuatwa na viongozi, ameongeza. "Hakuna sababu ya kuwa hofu au kusitisha shughuli za kiuchumi, tunafanya kilicho chini ya uwezo wetu kudhuibiti ugonjwa huo hatari," amesema.

Ugonjwa wa Marburg ni ugonjwa mkali wa wanadamu na wanyama kama vile tumbili, nyani, sokwe, ambao husababishwa na virusi vya Marburg vya aina mbili.

Ugonjwa huo husababishwa na virusi vinavyohusianishwa na Ebola na hata dalili zake hazina tofauti kubwa na ugonjwa wa Ebola.Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kikohozi, maumivu ya viungo, kuhara na kutapika, na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.

Ugonjwa wa Marburg ni nini?

Mlipuko huo ulitokana na tumbili wa Kiafrika walioagizwa kutoka Uganda. Lakini virusi hivyo vimehusishwa na wanyama wengine tangu wakati huo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt, Ujerumani na Belgrade huko Serbia.

Na miongoni mwa wanadamu, huenezwa zaidi na watu ambao wamekaa kwa muda mrefu katika mapango na migodi iliyo na popo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.