Pata taarifa kuu

Ugonjwa wa virusi vya Marburg waua tisa Equatorial Guinea

Watu tisa wamefariki kutokana na ugonjwa wa virusi vya Marburg, homa kali inayoambatana na kuvuja damu inayoua kama Ebola, mashariki mwa Guinea ya Ikweta, nchi ndogo ya Afrika ya kati ambayo imeweka karantini mkoa kunakoripotiwa ugonjwa huo ili kudhibiti "mlipuko" huo, Waziri wa Afya wa Equatorial Guinea alitangaza siku ya Jumatatu.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt, Ujerumani na Belgrade huko Serbia.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt, Ujerumani na Belgrade huko Serbia. © CDC/ Dr. Frederick Murphy
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, serikali ilitangaza kuwa inachunguza visa vinavyoshukiwa vya homa ya kuvuja damu. Ni watu watatu pekee walio na "dalili ndogo" za ugonjwa huo ambao wamewekwa karantini kwa wakati huu katika hospitali katika eneo hili lenye wakazi wachache na vijijini, linalopakana na Gabon na Cameroon, alisema Bw. Mitoha Ondo'o Ayekaba wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Watu watatu waliolazwa hospitalini "wana dalili ndogo na  wanaendelea kupata matiabu", aliongeza. Equatorial Guinea "inatangaza leo tahadhari ya afya ya homa ya kuvuja damu ya virusi vya Marburg katika jimbo la Kie-Ntem na katika wilaya (jirani) ya Mongomo", alibainisha waziri huyo.

"Mpango wa kukinga umewekwa" kwa ushirikiano wa karibu na Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa (WHO) "kukabiliana na janga hili" katika eneo hili lililofunikwa na msitu mnene wa Ikweta mashariki mwa nchi hii ambayo pia inajumuisha visiwa vikuu viwili.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kikohozi, maumivu ya viungo, kuhara na kutapika, na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.

Ugonjwa wa Marburg ni nini?

Mlipuko huo ulitokana na tumbili wa Kiafrika walioagizwa kutoka Uganda. Lakini virusi hivyo vimehusishwa na wanyama wengine tangu wakati huo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt, Ujerumani na Belgrade huko Serbia.

Na miongoni mwa wanadamu, huenezwa zaidi na watu ambao wamekaa kwa muda mrefu katika mapango na migodi iliyo na popo.

Je, inaeneaje?

Popo wa matunda aina ya rousette wa Misri mara nyingi huwa na virusi. Nyani wa kijani kibichi na nguruwe wanaweza pia kubeba.

Miongoni mwa wanadamu, huenea kupitia maji ya mwili na malazi yaliyochafuliwa nao.

Na hata watu wakipona, damu au shahawa zao, kwa mfano, zinaweza kuwaambukiza wengine kwa miezi mingi baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.