Pata taarifa kuu

Tanzania yachunguza ugonjwa wa ajabu ulioua watu 5

Tanzania imewataka wataalam wa matibabu kuchunguza ugonjwa wa ajabu 'unaoambukia' ambao tayari umeua watu watano nchini humo, mamlaka imesema.

La leptospirose est une zoonose très répandue dans le monde, particulièrement en milieu tropical, transmise par les rats.
La leptospirose est une zoonose très répandue dans le monde, particulièrement en milieu tropical, transmise par les rats. © Shutterstock / PattyPhoto
Matangazo ya kibiashara

Ugonjwa huu uligunduliwa kwa "watu saba wenye dalili kama vile homa, kutapika, kutokwa na damu na kushindwa kwa figo", imeeleza Wizara ya Afya katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Alhamisi jioni.

Wataalamu wa tiba wametumwa katika mkoa wa Kagera (kaskazini-magharibi) unaopakana na Uganda kuchunguza ugonjwa huu 'unaoambukia', amesema afisa wa afya, Tumaini Nagu.

"Sampuli zilichukuliwa kutoka kwa wagonjwa na watu waliofariki ili kubaini chanzo na aina ya ugonjwa huo," amesema katika taarifa, akitoa wito kwa watu kuwa watulivu.

Kisa hiki kinakuja baada ya mlipuko wa virusi vya Ebola nchini Uganda, ambao ulidumu karibu miezi minne na kuua watu 55. Uganda ilitangaza janga hilo mwezi wa Januari mwaka huu.

Mwaka jana, Tanzania ilibaini ugonjwa wa Leptospirosis, au 'ugonjwa wa panya' ambao uliua watu watatu katika mkoa wa Lindi (kusini mashariki).

Ugonjwa huu wa bakteria, unaoambukia kwa wanadamu na baadhi ya wanyama, huenea kupitia maji au chakula kilichochafuliwa na mkojo wa wanyama walioambukizwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.